Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Henry Kilewo atoa msaada wa mabati kwa wahanga wa mafuriko Kata ya Jipe jimboni Mwanga, Kilimanjaro

Kileo1

“Ni washukuru wote waliofanikisha safari yangu ya Mwanga ya kutembelea wahanga wa mafuriko katika kijiji cha Ruru Kata ya Jipe Jimbo la Mwanga, Ahsanteni wote watu wa Mwanga wamepokea ahsante yenu kwa faraja kubwa sana, Ni kweli ilikuwa ni safari ndefu ila mimi naamini ni safari fupi sana, Tuliweza kutoa mabati mpaka kwa Mwenyekiti wa UWT wa Kata bila kujali itikadi ya vyama, nilisimama na utu zaidi…”

Sehemu ndogo ya maneno ya shukrani toka kwa Henry Kilewo, (mwenye kombati nyeusi anaekabidhi mabati) ambae ni Katibu wa Chadema Kanda Maalumu ya Kinodnoni Dar es Salaam kufuatia ziara yake Wilayani Mwanga (nyumbani kwao) alipoenda kuwajulia hali wahanga wa mafuriko kijiji cha Ruru, Jipe mapema wiki hii.

Kileo2Henry Kilewo akizungumza na wananchi wa Kata ya Jipe, kijiini Ruto Wilayani Mwanga

Kileo3Bahati David (kulia) aliyeambatana na Henry Kilewo katika ziara hiyo wakisaidia na mwananchi wa Kata ya Jipe kujaza upepo kwenye tairi ya gari waliyokuwa wakisafiria kwa kutumia pump ya baiskeli.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO