Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Ziwa Manyara hatarini kutoweka

HIFADHI ya taifa ya Manyara ipo katika utafiti wa kina kulinusuru Ziwa Manyara ambalo lipo hatarini kutoweka kutokana na kujaa tope.

Hali hiyo imesababisha maji kukauka kipindi ambacho mvua hazinyeshi, hivyo kupunguza baadhi ya vivutio vya hifadhi hiyo.

Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano muhifadhi utalii katika hifadhi hiyo Jully Minja alisema hali hiyo kwa kiasi kikubwa imesababishwa na uharibifu wa mazingira unaotokana na kilimo kisicho na mpangilio kwenye maeneo ya mabondeni.

Alisema kutokana na hali hiyo mabonde na mito ambayo hutiririsha maji kuingia ziwani humo pindi mvua zinaponyesha husomba udongo mwingi na mchanga na kuuelekeza ndani ya ziwa hilo.

Minja alisema, hicho ndicho chanzo cha kuharibika kwa ziwa hilo.

Alifafanua kuwa hivi sasa zinahitajika jitihada za kina katika kufanya utafiti makini kulinusuru ziwa hilo ambalo limepungua kina chake kwa kiwango kikubwa.

Kutokana na hilo alisema maeneo mengi ndani ya hifadhi hayana maji kabisa.

“Hili ziwa lipo toka miaka ya 1960 wakati hifadhi hii inaanzishwa rasmi ambapo katika maeneo yanayozunguka hifadhi hii kulikuwa na wanyama wa kutosha ikiwemo simba faru, tembo, nyati, chui, pundamilia, twiga na wanyama wengine wa porini, lakini kutokana na binadamu kuongezeka katika maeneo haya na kuvamia hifadhi kuna baadhi ya wanyama wametoweka kabisa ikiwamo faru,’’ alisema mhifadhi Lyimo.

Naye Mhifadhi, Wiliam Daniel, alisema kutokana maji ya ziwa hilo kupungua imesebabisha ndege aina ya flamingo ambao walikuwa ni kivutio kikubwa nao kutoweka.

Alishauri kama utafiti utachukua muda mrefu hadi kupata suluhu ya tatizo hilo basi kama nchi tuanze kujiandaa kwa ajili ya kutangaza utalii mpya wa kutaka jamii ifike kutembelea ziwa lililopotea.

“Unajua tatizo hapa ziwa hili halina sehemu ya kutolea maji yanapoingia hivyo maji ya mvua yakiingia na tope vyote hujaa ndani ya ziwa bila kutoka hivyo sasa kina kinazidi kupungua na mtu kama hafahamu zikinyesha mvua kidogo anaona ziwa limejaa kumbe tope ndilo limezidi,’’ alisema Mhifadhi Daniel.

Ziwa hilo lilianza kupungua kina cha maji toka mwaka 1923 na sasa ongezeko limekua kubwa hali ambayo inahatarisha kutoweka.

Hifadhi hiyo ya Manyara ambayo ni ya pili kuanzishwa hapa nchini ikitajwa kuwa ni moja kati ya hifadhi kubwa zinazoliingia taifa fedha za kigeni kupitia utalii unaotokana na vivutio vya ziwa hilo na simba ambao hupanda miti.

Imeandikwa na Ramadhani Siwayombe, Arusha – kupitia Tanzania Daima 21Novemba 2012. Picha na http://tembeatz.blogspot.com

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO