Pingamizi lililowekwa na upande wa wajibu rufani kupitia Wakili wao Alute Mughwai ili rufaa ya Lema kupinga kuvuliwa ubunge isisikilizwe limetupiliwa mbali na Mahakama ya Rufaa baada ya kuridhika kwamba kosoro zilizolalamikiwa zilikuwa kwa upande wa Mahakama.
Pia kifungu kilichomhukumu Lema kina maksoa hivyo kesi itatajwa tena baada ya siku 14 kwa ajili ya kuendelea kusikiliza hoja za walio kata rufaa.Mawakili wa Mh Godbless Lema wanahitajika kutimiza mahitaji fulani ya kisheria ndani ya siku 14 ili shauri la rufaa hiyo iweze kupangiwa siku ya kusikilizwa na kuamuliwa.
Wadaiwa kwenye shauri hilo ni wanachama watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mkanga, Agness Mollel na Happy Kivuyo, waliofungua shauri lililotengua ubunge wa Lema wakidai kuwa wakati wa kampeni alimdhalilisha mgombea wa CCM, Dk. Batilda Burian kwa kutumia lugha za matuLema anawakilishwa na Wakili Method Kimomogoro, anayesaidiana na Tindu Lissu.
Baadhi ya wananchi, wapenzi wa Chadema wakimlaki Mh Lema mara baada ya kuwasili katika viwanja vya mahakama.
Jopo la Majaji likiwa tayari kuanza kazi
Wananchi na viongozi wakiingia kuandikisha chumba cha mapokezi katika Ofisi ya Chadema Kinondoni, Dar es Salaam.
1 maoni:
Hongera Lema, Chadema ni noma hawatuwezi, ng'o!
Post a Comment