Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Taarifa ya BBC: Matokeo yaanza kutolewa Marekani; Obama ashinda katika majimbo ambayo yalikuwa muhimu sana kubaini mshindi

Matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Marekani yameanza kutolewa kutoka maeneo mbali mbali ya nchi.
Hesabu ya Kura
Rais Barack Obama ameshinda katika majimbo ambayo yalikuwa muhimu sana kubaini mshindi wa uchaguzi huu ambayo ni Michigan na Pennsylvania, pamoja na mengine ambayo alishinda katika uchaguzi wa mwaka 2008.
Mwenzake wa Republican Mitt Romney ameshinda katika majimbo mengine muhimu pia ya Republican pamoja na kushinda Indiana ambalo lilimuunga mkono Obama mwaka 2008.
Kura za maoni kabla ya kufanyika uchaguzi huu zilionyesha kinyang'anyiro kitakuwa kikali ingawa zilimpa ushindi wa kura chache tu Rais Obama katika majimbo kadhaa muhimu.
Vituo vya kupigia kura vilianza kufungwa mapema katika maeneo ya Mashariki mwa nchi , huku majimbo ya Virginia na Ohio nayo yakifunga mapema.
Kwa sasa kura za Electoral College zinaonyesha Obama yuko nyuma ya Romney kwa kura sita
Wapiga kura waliofika mapema kupiga kura zao
Mamilioni ya watu walijitokeza kupiga kura siku ya Jumanne. Mshindi huenda akajulikana baada ya masaa kadhaa kuanzia sasa hususan huku matokeo katika majimbo mengine muhimu yakitolewa.
Kujua matokeo yalivyo hadi sasa tembelea  BBC Swahili sasa
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO