Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

WACHEZEA KICHAPO CHA MBWA MWIZI BAADA YA KUMFAYIA VURUGU WENJE AKIKABIDHI MADAWATI, MNYIKA ALIPA AHADI ALIYOITOA MKUTANO WA MWEZI WA 4 KUCHANGIA MADAWATI

Mbunge Mnyika akikabidhi kiasi cha shilingi laki moja kwa mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje kutimiza ahadi aliyoahidi kwenye mkutano uliofayika tarehe 7 mwezi wa 4, 2012  kuchangia madawati kwa shule za msingi wilaya ya Nyamagana ambapo nyingi ziko katika hali mbaya kwa wanafunzi wake wengi kuketi chini kwenye vumbi na mawe.

 

Mbunge wa jimbo la Nyamagana jijini Mwanza Ezekiel Wenje akihutubia wananchi waliofurika kwenye uwanja wa Sahara,  ambapo pia mbunge huyo alitumia fursa ya mkutano huo kukabidhi madawati 400 yaliyotengenezwa kwaajili ya kutatua tatizo la madawati kwa shule za msingi jijini Mwanza. 


Pichani ni baadhi ya madiwani wa CHADEMA kwa  kata mbalimbali jijini Mwanza pamoja na makada wa chama hicho waliohudhuria kusanyiko hilo kwenye uwanja wa Sahara leo jioni hapa jijini Mwanza.

Mnamo tarehe 7 mwezi 4 mwaka huu chama hicho kiliendesha harambee kwenye uwanja huu wa Sahara hivyo madawati haya ni matokeo ya changizo lililofanyika kwa kishindo kwa wananchi kujitokeza kuchangia hadi shilingi ya mwisho akibani mwao lakini baadhi ya wadau wengi na wengine waheshimiwa wabunge wenye majina waliahidi kwenye mkutano huo wa mwezi wa nne mwaka huu lakini mpaka leo ambapo tunaelekea kuumaliza mwaka 2012 hawajatimiza ahadi zao licha ya kupigiwa simu na kufuatiliwa mara kwa mara... Hakika ni maswali kwa wananchi wa jimbo hili.

Jumla ya shilingi milioni 56 ikiwa ni ahadi na pesa taslimu zilipatikana kwenye changizo la madawati lililofanyika mnamo mwezi wa nne 2012 ambapo pesa cash iliyopatikana ni shilingi milioni 24 ahadi ambayo haijalipwa mpaka sasa ni shilingi milioni 32. Kujua wanaodaiwa na viwango vya madeni yao kwa ahadi za madawati.

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema taifa, John Heche akihutubia mkutanoni hapoKaribu na robo ya mwisho wakati Mnyika akielekea kuanza kuhutubia joto la timbwili timbwili la vurugu likatokea mara baada ya watu kadhaa waliosadikika kuwa walikuwa wametumwa na maadui wa Wenje ambao wamo ndani ya chama hicho kufanya vurugu kwenye mkutano huo kwa kurusha mawe kwenye kusanyiko hali ambayo ilisababisha baadhi ya waungwana kusambaratika wakihofia usalama wao.


Mdau akitweta mara baada mvua ya makonde kumwangukia.. 


Huyu mwingine alikuwa akilia kwamba wamemfanyia uonevu kumpiga hata kumuumiza yeye ni mwanachama wa CHADEMA na hajatumwa na mtu. 


Hatimaye polisi walifanikiwa kufika eneo la kusanyiko haraka iwezekanavyo na kuwaondoa watu hao ambao walikuwa wakinyemelewa na wananchi wenye hasira kali licha ya kukumbilia kwenye jukwaa la viongozi.


Mbunge wa jimbo la Nyamagana jijini Mwanza Ezekiel Wenje akitoa maelekezo juu ya madawati hayo ambayo yametengenezwa kwa mtindo kuwa kila moja linauwezo wa kuketisha wanafunzi watatu.
Orodha ya shule zitakazo nufaika na mpango huo ni pamoja na Shule ya Lake A na B, Shule ya msingi Nyashana  A, B, na C,  Shule ya msingi Nyakabungo B, Mabatini A, B na C, Shule ya msingi Nyerere, Shule ya msingi Mandela, Ngwandu A, B, C na D, Nyagulugulu, Nyakato, Mahina, Mtakuja, Pamba, Hongera na nyingine ndani ya wilaya hiyo....  

Mbunge wa jimbo la Ubungo Mh. John Mnyika amelirudia neno lake lililompiga out Bungeni la kumtaja Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kuwa ni dhaifu. Akisema kwamba hapa hakuna mwongozo wa spika, hakuna utaratibu wananchi wamepiga kura....

PICHA ZOTE NA MELEZO: G. SENGO BLOG, MWANZA. BOFYA HIYO LINK KWA MATUKIO ZAIDI

seria signature

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO