Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MultiChoice Tanzania yatangaza punguzo la asilimia 10 kwa wateja wa huduma zake


Meneja Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw. Peter Fauel, akitangaza Punguzo la Asilimia Kumi ya Malipo ya mwezi kwa wateja wa Televisheni kwa Vipindi vya DStv likaloanza hapo kesho, ambapo amesema punguzo hilo litawawezesha wateja wao kulipia huduma za Matangazo ya Televisheni ya kituo hicho kwa gharama nafuu. Pia amesema Offer hiyo ya Punguzo la bei ni hatua ya Kampuni hiyo kurudisha fadhila kwa wateja wake kuelekea katika kipindi cha maadhimisho ya sikukuu za mwisho wa mwaka. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Barbara Kambogi na Kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Bi. Furaha Samalu.
*****
Kampuni ya MultiChoice imetangaza punguzo la asilimia 10 ya malipo ya mwezi kwa wateja wa televisheni kwa vipindi vya DStv litakaloanza leo Novemba 15, 2012.
Meneja Mkuu wa MultiChoice Tanzania, Peter Fauel alisema punguzo hilo litawawezesha wateja wao kulipia huduma za matangazo ya televisheni ya kituo hicho kwa gaharama nafuu.
Fauel alisema kwa wateja watakaokuwa wamelipia tayari huduma hiyo ndani ya mwezi huu, wataendelea kutumia hadi pale mwezi utakapokuwa umeisha, kisha wataanza na bei mpya ya punguzo kuanzia mwezi unaofuata ila wahakikishe huduma yao kutokatika.
"Tumedhamiria kuwapunguzia wateja wetu gharama kubwa kulingana na hali halisi ya maisha ya mwananchi wa kawaida," alisema Fauel.
Meneja mkuu huyo alisema, kuwa kama kawaida yao huwapa wateja wao unafuu wa bei kulingana na kipato chao, hivyo punguzo hilo litawanufaisha kwa kiwango kikubwa ili kila mmoja afaidi burudani.
Alisisitiza kuwa DStv itaendelea kuwapatia Watanzania na Waafrika kwa ujumla vipindi vyenye ubora kwa vile wamewekeza katika vipindi vipya.
Kwa wateja watakaonufaika na ofa hii, wataweza kupunguza gharama za kulipia huduma yao ya DStv kwa 150,000 kwa mwaka!
Fauel akaongeza kwamba “Tunawaahidi wateja wetu huduma bora na kwamba kwetu mteja ni mfalme. Mtandao wetu wa usambazaji unazidi kupanuka na sasa tupo kila mkoa wa nchi. Pia tunafurahi kwamba sasa tuna ofisi zetu Kariakoo na supermarket ya Uchumi iliyopo barabara ya Pugu. Hii itawarahisishia wateja wetu kupata bidhaa na huduma zetu kwa haraka zaidi.
Chanzo: Bashir Nkoromo


Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO