Mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi NEC mjini Dodoma, umempitisha Abdulhaman Kinana kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho tawala.
Mwenyekiti wa CCM, Mh Jakaya Kikwete alishamteua Katibu Mkuu wa zamani, Philip Mangula, kuwa Makamu Mwenyekiti, akirithi mikoba ya Pius Msekwa.Naye Mwigulu Nchemba amechaguliwa kuwa naibu katibu mkuu wa chama hicho upande wa bara na Vuai Ali Vuai upande wa Tanzania visiwani.
Wengine waliofanikiwa kupita kwenye secretarieti ya chama hicho ni pamoja na Asha Rose Migiro ambaye amechaguliwa kushughulikia masuala ya kimataifa na Zakhia Meghji amechaguliwa kushika nafasi ya uweka hazina.
Nape Nnauye ameendelea kushikilia nafasi yake katibu na uenezi wa chama hicho.
Abdurahman Kinana-Katibu Mkuu wa CCM
Mwigulu Nchemba-Naibu Katibu Mkuu CCM (Bara)
Vuai Ali Vuai-Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar)
Nape Nnauye-Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi
Asha-Rose Migiro-Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa
Zakia Hamdan Megji- Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha
Muhammed Seif Khatib-Katibu wa NEC, Oganaizesheni.
Picha zote kwa hisani ya Bashir Nkoromo
1 maoni:
Kazi ipo!
Post a Comment