Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

ASKARI WALIOMUUA SWETU FUNDIKIRA WAHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA

Askari wa JWTZ waliotiwa hatiani hii leo na Mahakama Kuu ya Tanzania kwa mauaji ya Swetu Fundikira, Koplo Ali Ngumbe (kushoto) na Sajini Rhoda Robert. Watuhumiwa hawa na mwenzao mmoja Mohamed Rashid wamehukumiwa Kunyongwa hadi kufa.

Marehemu Swetu Fundikira wakati wa uhaiwake akiwa na mkewe.

ASKARI wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Sajent Rhoda Robert, Koplo Ally Ngumbe na Mohamed Rashidi waliokuwa wakikabiliwa na Kesi ya mauaji ya Marehemu Swetu Fundikira hukumu yao imetolewa leo na Askari hao kuhukumiwa Kunyongwa hadi kufa.

Hukumu hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na ndugu jamaa na marafiki wa Swetu duniani kote ilitolewa leo katika Mahakama Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.

Washtakiwa hao watatu wametiwa hatiani baada ya kufanya kosa hilo siku ya Jumamosi tarehe 23 Januari, 2010 kwa kumpiga bila huruma Swetu Fundikira maeneo ya Kinondoni kwenye makutano ya barabara za Mwinjuma na Kawawa jijini Dar es salaam mpaka kusababisha kifo chake.

Baada ya kusomwa kwa hukumu hiyo vilio vimetawala kwa ndugu wa watuhumiwa hao huku baadhi ya watu wakidai sheria imechukua mkondo wake ipaswavyo.

Source: Raha za Pwani Blog

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO