Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

BAVICHA kupanda Mlima Kilimajaro Novemba 25–30, 2012 na kauli mbiu ya “VIJANA CHACHU YA MABADILIKO, TUNA MUNGU TUNA NGUVU”

akilimanjaro11Vijana wa Chama Cha Demokraisa na Maendeleo (CHADEMA) wanatarajiwa kupanda mlima mrefu kuliko yote Afrika, Mlima Kilimanjaro baadae mwezi huu kwa lengo kupandisha bendera ya chama chao kuunga mkono vuguvugu la mabadiliko nchini (M4C) sambamba na kuunga mkono utalii wa ndani.
Ziara hiyo inayoratibiwa na BAVICHA Mkoa wa Arusha inataraji kujumuisha vijana zaidi ya 200 ambao tayari wameonesha nia ya kutaka kushiriki.
Akizungumza na Blog hii, Mratibu Mkuu wa Ziara hiyo ambae ni  Mwenyekiti wa Vijana wa Chadema Mkoa wa Arusha, Mh Ephata Nanyaro amesema kuwa wazo la kupanda mlima huo walikuwa nalo muda mrefu lakini lilisitishwa kwa muda kupisha shughuli nyingine za kichama.
Safari yetu hii ina lengo la kuondoa HODHI ya mali za kitaifa ambazo kwa muda mrefu sasa zimekuwa zikishikiliwa (vikihodhiwa) na chama kimoja tu kilichopo madarakani, pia tutapandisha Bendera ya chama chetu juu kabisa ya mlima Kilimanjaro ili kuionyesha dunia kuwa tupo tayari kwa mabadiliko,na saa ya mabadiliko ni sasa” alisema Nanyaro
SAM_4465Akisisitiza zaidi Mh Nanyaro anasema “tumekubaliana kuwa tutaanza expedition hiyo Novemba 25 hadi Novemba 30, ili Decemba 1 tuwe tumesharudi tuweze kutembelea watu wanaoishi na VVU”
Nanyaro anasema maandalizi yote ya safari hiyo itakayowagharimu siku 6 za kuwa mlimani yanaendelea vizuri na kwamba wanawakaribisha wananchi wote watakaoamua kuwaunga mkono kwa safari yao hiyo.  Anasema fedha zote za kugharamia safari hiyo ni michango binafsi ya vijana hao ambao kila mmoja amechangis sh 50,000 tu!

Mratibu huyo anasema kwa watu ambao watakuwa wanatamani kujiunga nao katika safari hiyo wanakaribishwa na wanaweza kuwasiliana nae kwa nambari 0757 755 333 na kupatiwa maelekezo zaidi.
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO