Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Makamanda wa Chadema watikisa Mji wa Moshi

DSC07321Diwani wa Viti Maalumu  katika Manispaa ya Moshi, Hawa Mushi (Chadema), pamoja na Chris Mbajo (mwenye miwani) katika moja ya mikutano waliyoshiriki Wilayani Bababti mapema mwezi huu.

DSC05527Frank Oleleshwa

DSC05526Mwanasheria James Lyatuu

DSC06427Diwani hawa akiwa mwenye furaha katika moja ya mikutano ya Chadema Mjini Moshi mwezi uliopita. Picha zote ni za maktaba yetu

***************
MAKAMANDA wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutoka Jiji la Arusha, juzi walitikisa mji wa Moshi huku wakitaka wananchi kujiandaa kuchukua nchi kwa njia ya kura 2015.
Katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Aslam Gereji, Kata ya Mawenzi, makamanda hao pia walitaka wananchi kuishinikiza Serikali, ili irejeshe mabilioni ya shilingi yaliyofichwa Uswisi.

Chiristopher Mbajo anayetarajiwa kugombea Ubunge Same Magharibi mwaka 2015, alihoji uhalali wa vyombo vya dola vya Tanzania, kuwabebesha wananchi jukumu la vigogo walioficha fedha Uswisi.

“Jukumu la kumchunguza mwananchi wa kawaida au kiongozi ni la vyombo vya dola lakini leo Zitto (Kabwe-Mbunge Kigoma Kaskazini) anatakiwa eti apeleke majina hii ni aibu,”alisema Mbajo.
Wakili wa Jijini Arusha, James Lyatuu alisema ugumu wa maisha unaowakabili Watanzania hivi sasa kuliko awamu zote za Serikali ya CCM zilizotangulia, ndio silaha ya kuking’oa chama hicho katika uchaguzi wa mwaka 2015.

“Maisha wakati wa Rais Ali Hassan Mwinyi (1985-1995) na Benjamin Mkapa (1995-2005), yalikuwa mazuri kuliko ya Rais wa sasa Jakaya Kikwete, hakuna sababu ya kuendelea na CCM,”alisema.
Wakili huyo aliwataka wakazi wa Moshi, kusimama imara kudai haki yao ya kikatiba ya maisha bora na wale watakaopata misukosuko kwa kutetea haki yao, yuko tayari kuwatetea bure mahakamani.
Katibu Mwenezi wa Chadema katika Kata ya Sekei jijini Arusha, Bahati David alisema CCM ni wepesi kama pamba na kwamba chama hicho kijiandae kuwa chama cha upinzani katika uchaguzi mkuu wa 2015.

Kwa upande wake,Diwani wa Viti Maalumu  katika Manispaa ya Moshi, Hawa Mushi (Chadema), aliitaka CCM kujiandaa kukabidhi madaraka kwa Chadema kwa amani ifikapo mwaka 2015.
Diwani huyo ambaye ndiye aliyeandaa mkutano huo wa hadhara, alisema mafanikio ambayo Chadema Moshi imeyapata katika kipindi kifupi ni kielelezo cha umakini katika kusimamia maslahi ya umma.

Mwenyekiti wa zamani wa Umoja wa Vijana wa CCM (Uvccm)  Wilaya ya Simanjiro, Frank Ole Lelesho, alisema uendeshaji bora wa mji wa Moshi ni kielelezo cha umakini wa viongozi wa Chadema.

Kwa mujibu wa Ole Lelesho, wapo watoto waliozaliwa katika wilaya ya Simanjiro hadi wakamaliza kidato cha nne lakini hawajawahi kuona lami lakini mji wa Moshi una lami hadi pembezoni.

Imeandikwa na: Daniele Mjema; Mwananchi – Moshi, 26/11/2012

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO