Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mikopo elimu ya juu kugharimu bil. 326/-

na Rodrick Mushi, Moshi (Tanzania Daima)
NAIBU Waziri wa Elimu, Philip Mulugo, amesema serikali inatarajia kutoa mikopo yenye thamani ya sh bilioni 326 katika mwaka huu wa fedha kwa wanafunzi wa elimu ya juu kupitia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.
Mulugo alieleza hayo mwishoni mwa wiki mjini hapa kwenye mahafali ya tano ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mwenge (MWUCE) na kuongeza kuwa wanafunzi 98,772 wanatarajiwa kunufaika na mkopo huo.
Alisema fedha hizo zitatolewa kwa awamu ambapo mpango wa serikali ni kuendelea kuimarisha na kuboresha usimamiaji wa utoaji wa mikopo na urejeshwaji inayotolewa kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
Hata hivyo, alisema kuna ongezeko la wanafunzi wanaohitimu elimu ya juu kutoka wanafunzi 14 mwaka 1964 hadi kufikia wanafunzi 166,484 kwa mwaka 2011/2012 na ongezeko la vyuo kutoka chuo kimoja hadi vyuo 42.
Alisema vyuo binafsi ikiwemo Mwuce vimekuwa na mchango mkubwa katika kuleta maendelea nchini kwa kusaidia ongezeko la wataalamu ikiwemo sekta ya elimu.
Katika mahafali hayo, Mulugo alitoa sh milioni 10 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya mafunzo ya sayansi chuoni hapo ambavyo vilielezwa kuwa ni changamoto kubwa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya chuo hicho, Askofu Isaac Aman, alisema chuo kimekuwa kikikumbana na changamoto ya wanafunzi wanaohitimu elimu ya sekondari hususan kidato cha sita kutokuwa na sifa stahiki ya kujiunga na chuo.


Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO