Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

UADILIFU WA KINANA WAANZA KUTIA SHAKA

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, ambaye maisha yake kwa muda mrefu yamekuwa ayamulikwi na waandishi wa habari safari hii yameanza kuingia dosari baada ya kutangazwa rasmi kuwa Katibu Mkuu CCM.

Gazeti moja la wiki ndilo lililokuwa la kwanza kwa kuchapisha habari iliyomueleza kuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni iliyousika na usafirishaji wa meno ya tembo.

Duru nyingine za mambo ya siasa sina muusisha na utajiri uliyo kithiri pamoja na uhusianao wa moja kwa moja na Kampuni ya Kiarubu iliyoipewa sehemu ya Loliondo Kuwinda ambayo inapigiwa kelele na wanaharakati mpaka leo hii.

Binafsi Katibu Mkuu huyo wa chama tawala amesema hahusiki na usafirishaji wa meno ya tembo nje ya nchi.

Hata hivyo, amekiri kuwa mmiliki wa Kampuni ya uwakala wa meli ya Sharaf Shipping Agency, iliyohusika kusafirisha makontena yaliyokuwa na nyara hizo za serikali, kabla ya kukamatwa nchini China yakiwa safarini kupelekekwa Hong Kong.

Gazeti hilo lilimtaja Kinana kuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo kwa kuwa na hisa 7,500 kati ya 10,000 katika kampuni hiyo, huku hisa nyingine 2,500 zikiwa zinamilikiwa na mshirika mwenzake, Rahma Hussein. Thamani ya hisa hizo ni sh 1,000 kila moja.

Kinana akitoa ufafanuzi kuhusiana na hilo alishanga kuhusishwa na meno hayo. “Nimeisoma habari hiyo na kwa bahati mbaya sioni anayenilaumu wala kitu ninacholaumiwa nacho. Kwamba nina hisa katika kampuni ya wakala wa meli ya Sharaf ni kweli.

“Lakini mimi sina nafasi yoyote ya kiutendaji na wala sishughuliki na uendeshaji wa kampuni hiyo. Kwa kweli sikujua na wala sikuhusika kwa namna yoyote ile na usafirishaji wa makontena hayo na mengine yoyote,” alisema Kinana.

Alifafanua kuwa, wenye wajibu na mamlaka ya kukagua shehena zote zinazosafirishwa nje ya nchi ni mamlaka za serikali na si kampuni ya uwakala wa meli.

Alisisitiza kuwa, hana mamlaka kwa mujibu wa sheria kukagua mali inayosafirishwa japokuwa anaweza kuuliza bidhaa iliyopo katika makontena hayo. “Ni dhahiri kabisa kwamba, habari hii imeandikwa na jina langu kutumika katika malengo ambayo siyajui. Nahisi kama jina langu limetumika kama pilipili katika kachumbari ili kunogesha habari.

“Kwa bahati mbaya pilipili imezidi katika kachumbari. Kama lengo lilikuwa kupasha habari, basi umma umedanganywa,” alisema Kinana. Kwa mujibu wa habari hiyo, sakata la kukamatwa kwa nyara hizo za serikali liliibuliwa kwa mara ya kwanza na Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela, katika Bunge lililopita la bajeti.

Posted by JAMII Blog on 18 November, 2012

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO