Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

KIKWETE AZINDUA UKUMBI WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI (EALA) JIJINI ARUSHA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akilihutubia Bunge la Afrika Mashariki wakati alipofika kuzindua Ukumbi Mpya wa Bunge la Afrika Mashariki ulioko katika jengo jipya la Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha.

Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akimpokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipokuwa akiwasili katika jengo jipya la Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha kwa lengo la kuzindua Ukumbi wa Bunge la Afrika Mashariki ulioko katika jengo hilo.

Spika wa Bunge la Africa Mashariki Mhe. Margret Natongo Zziwa (kulia) akimkaribisha Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda katika jengo hilo.

Spika wa Bunge Afrika Mashariki,Mhe. Margret Natongo Zziwa akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) ili kulihutubia Bunge la Afrika Mashariki.Kulia ni Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda.

Baadhi ya Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Rais Jakaya Kikwete.

Jengo jipya la Jumuiya ya Afrika Mashariki.Picha na Prosper Minja- Bunge

PICHA KWA HISANI YA : WAZALENDO 25 BLOG

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO