Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TUME YA KATIBA YAKUSANYA MAONI WILAYANI KARATU

Mkazi wa kijiji cha Slahhamo Kata ya Mbulumbulu Wilaya ya Karatu mkoani Arusha, Thimos Mushi (51) akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya wakati wa mkutano wa kukusanya maoni ulioitishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kijijini hapo.

Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bi. Mwantumu Malale (kushoto) akisalimiana na Katibu Tarafa wa Kata ya Mbulumbulu Wilayani Karatu mkoani Arusha, Tatu Eliasi jana jumatatu Novemba 19, 2012 wakati wajumbe wa Tume hiyo walipofika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Karatu kabla ya kuanza kazi ya ukusanyaji maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya Wilayani humo. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Daudi Ntibenda

Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Charles Masero (mwenye shati jeupe) akitoa ufafanuzi kuhusu ujazaji wa fomu za maoni kuhusu Katiba Mpya kwa wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi cha Audry Veldan kilichopo kijiji cha Shahhamo Kata ya Mbulumbulu Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha wakati wa mkutano wa kukusanya maoni ya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya kijijini hapo.

Akina Mama wa kijiji cha Slahhamo Kata ya Mbulumbulu Wilaya ya Karatu mkoani Arusha wakisoma nakala za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba katika lugha nyepesi wakati wa mkutano wa kazi ya ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya ulioitishwa na Tume  ya Mabadiliko ya Katiba kijijini hapo.

Wananchi wa Kata ya Rhotia Wilaya ya Karatu mkoani Arusha wakifuatilia mkutano wa kukusanya maoni kuhusu Katiba Mpya uliotishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika Kata hiyo

CHANZO: HAKINGOWI.COM

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO