Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Di Matteo amebaki historia Chelsea

Mmiliki huyo wa Chelsea, amekasirishwa na matokeo mabaya ya Chelsea katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, na kumfukuza kazi Mtaliano Di Matteo baada ya timu hiyo kuzabwa mabao 3-0 na Juventus juzi, ikiwa ni miezi sita tu tangu aipe timu hiyo taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Sasa mtu wa kwanza kabisa ambaye Abramovich anamtaka akarithi mikoba ya Mtaliano huyo ni kocha wa zamani wa Barcelona, Pep Guardiola, na kama akikwama kwa Mspanyola huyo ambaye amesema hataki ukocha tena kwa sasa, basi atahamishia ndoana zake kwa Rafa Benitez.

MAKOCHA WALIODUMU MUDA MFUPI CHESLEA:

Guus Hiddink         Siku 105

Felipe Scolari         Siku 223

Avram Grand          Siku 247

Andre Villas-Boas   Siku 256

Roberto Di Matteo   Siku 262

MATOKEO YALIYOMFUKUZISHA KAZI DI MATTEO:

Oktoba 23: Shakhtar 2 Chelsea 1        (Ligi ya Mabingwa)

Oktoba 28: Chelsea 2 Man United 3    (Ligi Kuu)

Oktoba 31: Chelsea 5 Man United 4    (Kombe la Ligi)

Novemba 3: Swansea 1 Chelsea 1      (Ligi Kuu)

Novemba 7: Chelsea 3 Shakhtar 2      (Ligi ya Mabingwa)

Novemba 11: Chelsea 1 Liverpool 1     (Ligi Kuu)

Novemba 17: West Brom 2 Chelsea 1  (Ligi Kuu)

Novemba 20: Juventus 3 Chelsea 0     (Ligi ya Mabingwa)

Taarifa hii ni Kwa Hisani ya Bin Zubeiry Blog

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO