Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

WALIOKUWA MADIWANI WA CHADEMA WALIPISHWA FAINI YA MILIONI 15 AMA KIFUNGO GEREZANI

 

HATIMAYE hukumu ya  kesi ya madai iliyokuwa ikiwakabili  waliokuwa madiwani watano wa  chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) hukumu yake imesomwa ambapo Mahakama imeamuru madiwani hao kulipa kiasi cha shilingi milioni 15 kwa awamu mbili na endapo kama watashindwa kulipa
fedha hizo basi watapelekwa magereza.

Akitoa hukumu hiyo mbele ya Umati wa watu ambao walikuwa wamefurika Mahakamaani hapo mapema jana (juzi) katika Mahakama Kuu kanda ya Arusha, Charlz Magesa alisema kuwa rufaa imefika mwisho.

Magesa alisema kuwa washitakiwa hao ambao  walikuwa madiwani wa kata tano za jiji la Arusha wamekutwa na hatia hivyo Mahakama imeamuru walipe kiasi hicho cha fedha haraka iwezekanavyo na endapo kama watashindwa kufanya hivyo basi watachukuliwa hatua kali ikiwemo kupelekwa magereza.

Aliongeza kuwa kwa sasa Madiwani hao wanatakiwa kulipa fedha hizo kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza itakuwa ndani ya wiki mbili wakati awamu ya pili itakuwa ya mwisho na nibaada ya miezi miwili.

‘kwa sasa mnatakiwa muhakikishe kuwa mnalipa fidia kwa haraka sana na kama mtashindwa kufanya hivyo basi mahakama itachukua hatua na maamuzi makali zaidi ya haya’aliongeza Magesa

Wakiongea nje ya Mahakama mara baada ya kukubaliana kulipa kiasi hicho cha fedha madiwani hao ambao walikuwa mahakamani hapo ambao ni Rehema Mohamed, Charlz Mpanda,na Rubeni Ngowi walidai kuwa Chadema haijawatendea haki kwa kuwa fedha ambazo wanatumia kumlipa Wakili ili kuwakandamiza ndizo walizozitafuta kwa kipindi cha hapo awali.

Madiwani hao waliongeza kuwa wao wapo tayari kulipa hizo gharama kwa ndiyo haki ambayo Chadema walikuwa wanaililia hivyo wameomba Viongozi wa Taifa watafute njia nyingine ya kutatua migogoro na wala sio kufukuza  kwani inapoteza imani na chama.

‘ukiangalia hapa tunaambiwa kuwa tulipe kiasi hiki cha fedha lakini nguvu zetu bado hazijalipwa na sisi ndio tuliotangaza Chadema kwa mkoa wa Arusha na mpaka sasa kila mtu anaijua Chadema lakini malipo yake ndiyo haya sisi tunasema kuwa huu si mwisho wa siasa bado tupo na tutakutana katika gemu nyingine ‘waliongeza madiwani hao

Pia walisema kuwa pamoja na kuwa baadhi ya waliokuwa madiwani hawataki siasa lakini bado wengine wataendelea tena kwa kishindo kikubwa hata kama Chadema wanadai kulipwa fedha zao na Kata zao zikiwa zinabaki hazina madiwani kwa muda mrefu sana.

Awali kesi hiyo ilitokana na madiwani hao kufungua kesi ya kupinga kufukuzwa na kuvuliwa uanachama baada ya kudaiwa kukiuka sheria na kanuni za chama, zikiwemo sheria za kuwataka kutoingia katika vikao
vya madiwani vya Jiji la Arusha kwa madai ya kutomtambua Meya wa Arusha Gaudence Lyimo wa Chama cha Mapinduzi(CCM)

Chanzo: Libeneke la Kaskazini

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO