Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Breaking News: Wananchi wa Mbeya Mjini wamezuia magari yote yanayosafirisha mafuta kwenda nje ya nchi kwa madai kwamba hawawezi kukubali mafuta yapite kwao huku wao wakitaabika kwa kukosa mafuta kwa magari yao!!

Blog hii imepokea taarifa muda huu ikieleza kuwa hali ni tete katika Jiji la Mbeya baada ya wananchi Jijini hapo kuamua kuweka mawe barabarani kuzuia malori yanayosafirisha mafuta kwenda nchi za Zambia, Kongo n.k yasiendelee na safari baada ya kuona kero ya kukosa mafuta kwa ajili ya magari yao ikikosa ufumbuzi ilahali wanashuhudia mafuta hayo yakipita kwenda nchi za wengine.
Zifuatazo ni baadhi ya picha za tukio hilo lililodumu kwa takriban saa moja kabla ya wanausalama hawajaingilia kati na kutuliza hali katika eneo la Kwa Mama John Jijini Mbeya. Picha hizi ni kwa mujibu wa MBEYA YETU BLOG
SHUKRANI KWA MBEYA YETU BLOG
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO