
Kutoka kushoto, Mbunge wa Arumeru Mh Joshua Nassari, aliekuwa Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema, Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha, Mh Amani Golugwa na Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa Mh John Heche wakiwa sehemu ya wageni muhimu katika mkutano wa hadhara kufunga kampeni za kuwania nafasi ya kuongoza mitaa tisa katika Halmashauri ya Mji mdogo wa Usa River – Arumeru Mashariki.
Kampeni hizo za Chadema zilihitimishwa jana katika uwanja wa Shule ya Msingi Usa ambapo wananchi walijitokeza kwa wingi sana. Leo Jumapili Novemba 4, 2012 uchaguzi huo unafanyika, na kwa mujibu wa Katibu wa Chadema Mkoa, Amani Golugwa, Chadema wamedai kujipanga kushinda mitaa yote sita ili kuweza kumsaidia Nassari ambae ni mbunge kutoka chama hicho kufanikisha utekelezaji wa mipango yake ya maendeleo kama Mbunge wa Jimbo hilo.

Kwa siku ya jana Chadema walifanikiwa kufanya mikutano mingine minne ya kawaida maeneo tofauti ya Mji wa Usa chini ya Ally Bananga ambae alitokea kuwa kivutio kwa watu wengi, akisaidiana na Mbunge wa Arumeru Mashariki Mh Joshua Nassari kabla ya kuhitimisha kwa mkutano mkubwa katika viwanja hivyo vya shule ya Msingi Usa.

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Mh Joshua Nassari akiongea na wananchi katika mkutano wa jana Usa River na kuwataka wananchi hao wamsaidie kupata viongozi hao wa mitaa watakaomsaidia kukamilisha ahadi mbalimbali za kuboresha maisha ya watu wake Jimboni humo.

Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa, John Heche akihutubia katika kutano huo ambapo aliwataka wananchi hao kutopoteza nafasi hii adimu ya kumuongezea nguvu Mbunge wao Joshua Nassari (CHADEMA) kwa kumchagulia wagombea hao wa tisa wa Chadema kumsaidia.

Mbunge Joshua Nassari akiwasili viwanjani hapo na kulakiwa na wananchi kwa shangwe kama picha inavyoonesha.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha, Amani Golugwa akisisitiza jambo katika mkutano huo jana

Godbless Lema, ambae uamuzi wa rufaa yake unatarajiwa kutolewa baadae Novemba 8, 2012 Mahakama kuu Jijini dar es Salaam, nae alipata wasaa wa kuzungumza katika kkutano huo.

Mdau wa Blog hii akiteta jambo na Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha, Amani Golugwa wakati mkutano unaendelea jana katika uwanja wa Shule ya Msingi Usa River
SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
BONYEZA LINK HAPA KUSOMA STORI HIZI PIA
0 maoni:
Post a Comment