Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

RAIS KIKWETE NA VIONGOZI WENZIE WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAZINDUA BARABARA YA ARUSHA-NAMANGA-ATHI RIVER

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi Kenya Jumatano Novemba 28, 2012 tayari kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa barabara ya Arusha-Namanga-Athi River pamoja na Mkutano wa Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utaozungumzia maendeleo ya miundombinu. 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi Kenya Jumatano Novemba 28, 2012 tayari kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa barabara ya Arusha-Namanga-Athi River pamoja na Mkutano wa Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utaozungumzia maendeleo ya miundombinu.Kulia ni Balozi wa Tanzania Nchini Kenya,Mh. Batilda – Salha Burhan.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete (wa pili kushoto) akiwa katika mazungumzo na Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ismailia Mtukufu Aga Khan (kushoto) katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi Kenya Jumatano Novemba 28, 2012.Rais Kikwete yupo nchini Kenya kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa barabara ya Arusha-Namanga-Athi River pamoja na Mkutano wa Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utaozungumzia maendeleo ya miundombinu.Wengine Pichani ni Rais wa Kenya,Mh. Mwai Kibaki (katikati) na Rais wa Burundi,Mh. Nkurunzinzah.

Wakati wa Wimbo wa Taifa.

Baadhi ya mawaziri na makatibu wakuu wa Tanzania waliohudhuria sherehe za uzinduzi rasmi wa barabara ya Arusha – Namanga – Athi River yenye urefu wa kilometa 104.4 kwa upande wa Tanzania.

Baadhi ya Maafisa wa Jeshi la nchini Kenya wakiwa kwenye Sherehe hiyo.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia kwenye sherehe za ufunguzi wa barabara ya Arusha-Namanga-Athi River

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakipata maelezo ya Barabara hiyo itakavyokuwa kutoka kwa Injinia.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakikata utepe kwa pamoja kuzindua rasmi wa Barabara ya Arusha – Namanga – Athi River yenye urefu wa kilometa 104.4 kwa upande wa Tanzania.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali waliofanikisha ujenzi wa barabara ya Arusha – Namanga – Athi River. PICHA NA IKULU via IKULU BLOG

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO