Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Uzembe huu ni hatari kwa usalama wa watu Mahakama Kuu Arusha

DSCN6295Kamera yetu mapema leo asubuhi iliweza kunasa tukio linaloashiria hali ya hatari kwa usalama wa wananchi wanaokwenda Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kwa shughuli mbalimbali. Kinachoonekana pichani ni kipande cha mbao “fascia board” kwa lugha ya wajenzi, ambacho kinaning’inia juu baada ya kupoteza uimara katika moja ya majengo ya Mahakama hiyo. Kipande hiki kikidondoka na kukuta mtu au mali yeyote chini ni rahisi kuleta uharibifu na madhara mengineyo. Haijaweza kufahamika mara moja kama hitilafu hii ya kiujenzi inafahamika na wahusika wanaosimamia majengo ya Mahakama :Estate Managers’ Department” kama ipo.

DSCN6296

DSCN6294Wananchi wakikatiza jirani kabisa na mahali hapo, na wakati mwingine kuna magari yanaegesha kwa chini yake. Blog hii inatoa wito kwa wahusika kuifanyia kazi dosari hii ambayo kama madhara yatatokea basi sababbu kubwa itakuwa ni uzembe.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO