Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Diwani wa Chadema Arusha aanika ufisadi wa kutisha katika shughuli ya uzinduzi wa Jiji la Arusha

OFISI YA KATA LEVOLOSI
TAARIFA KWA UMMA, UKWELI JUU YA UFISADI WA KUTISHA UZINDUZI WA JIJI.
Nimesikitishwa sana na taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha kwa vyombo vya habari 17/11/2012, taarifa hii imejaa uongo wa kiwango cha kutisha,na ambayo haipaswi kutolewa na mtu mwenye dhamana ya ofisi ya umma,ni wazi imelenga kuficha ukweli,na ni wazi Mkurugenzi amelazimishwa kuitoa si kwa utashi wake bali kwa waliomtuma ili kuendelea kulinda genge ambalo limekuwa kwa muda mrefu likiendesha Halmasahuri.Taarifa hii haina hata chembe ya ukweli, wala haina maslahi kwa umma wa Arusha na nchi kwa ujumla ambao kodi zao zimetumiwa kifisadi,ni wazi ofisi hii ya mkurugenzi na Mkurugenzi mwenyewe imeendelea kutumika kisiasa kwa mara nyingine tena
Ni kweli sherehe zilifanyika kutokana na kupatikana kwa jiji,hakuna kokote ambako mimi binafsi au chama changu tumenukuliwa tukipinga sherehe za uzinduzi kufanyika,bali tunapinga UFISADI wa kutisha kwenye sherehe za uzinduzi wa jiji,haiwezekani jiji linalokabiliwa na changamoto nyingi kutumia zaidi ya Sh 123,689,550 kwa ajili ya sherehe za uzinduzi.Haijalishi wapi fedha zimetoka,hoja ya msingi ni kuwa matumizi haya ni ufisadi wa kiwango cha kutisha.Mkurugenzi kwa upofu wake na kundi lake anataka kuhalalisha matumizi haya kwa kigezo kuwa kuna wadau waliichangia Halmashauri,huu ni upofu wa kiwango cha kutisha
Matumizi ya Sh 114,149,500 ambayo ndio yaliyoletwa kwenye Baraza la madiwani ni BATILI kwa kuwa wakati kiwango hiki kinaletwa tayari malipo yalishalipwa, Tayari Sh 26mil zilishalipwa A to Z, Sh 12mil kundi la Orijino Comedy, Sh10mil msanii Diamond, ngoma za asili, nk. Kimsingi malipo haya yalifanyika kabla ya baraka za baraza la madiwani chombo chenye mamlaka ya kuidhinisha malipo. Katika malipo yaleyele ambayo Baraza lililetewa ndio haya haya a mbayo Mkurugenzi anadai kuwa kuna wadau walishayalipia
1.AUWASA Sh 18,156,500 kwa ajili ya ukarabati wa eneo la mnara wa azimio la Arusha
2.Jiangxi Geo Engeneering (Group) Corporation – Sh milioni 12
3.China Railway Seventh Group Ltd – Sh milioni 4
Kimsing kazi hizi zilifanywa na fedha kwa mujibu wa dokezo lililoletwa kwenye baraza na mweka hazina.Ni wazi kuwa huu ni UFISADI
Hakuna kokote ambako Mkurugenzi amewahi kupeleka kwenye baraza au kikao cha kamati ya fedha na utawala taarifa ya wadau hawa kuisadia Halimashauri,huu ni ufisadi wa kiwango cha juu
Kamati ya fedha na utawala ilipelekewa bajeti ya 66mil ambayo haikupitishwa na badala yake wajumbe wakataka ifanyiwe marekebisho,(HAIKUPITISHWA),badala yake baraza likaletewa 114,149,500mil ikakataliwa,badala yake leo tena baada ya kupiga kelele Mkurugenzi anadai imetumika 123,689,500mil,ambayo Baraza halijapitisha huu ni UFISADI na lazima hatua stahiki zichukuliwe,
Kwamba halimashauri inalipa 12mil kwa Orijino comedy ili kufanya mahojiano na vyombo vya habari ili kuwajulisha umma wa Arusha kuhusu uzinduzi wa jiji,huu ni WENDAWAZIMU na ufisadi wa kiwango cha juu.Ukweli ni kuwa awali Mkuu wa Wilaya alikubaliana na orijino comedy kwa 5mil,kwa nini Mkurugenzi na mweka hazina walilipa 7mil zaidi ya makubaliano ya DC na orijino comedy?
Ukweli kuhusu kamati ya chakula na ushiriki wangu,kwanza hakuna kamati ya chakula iliyoundwa inayowahusisha Madiwani,bali kwenye kikao cha baraza gharama ya chakula kwa wageni 200,ilikuwa 15mil,ukigawanya unapata wastani wa Tshs 75,000 kwa mtu mmoja,ambayo niliipinga kwa kuwa hakuna menu ya gharama hiyo kwenye hotel yoyote hapa Arusha hasa kama chakula ni Buffet,
Buffet ya ghali sana kwenye hotel husika ni Tshs 45,000.Kwa msingi huo ndio nikaingilia kati ili kuokoa fedha za walipakodi wa Arusha,na kamwe si kamati ya chakula kama ambavyo Mkurugenzi amedai.Kwa upofu wa hali ya juu Mafisadi hawa wanataka kubadilisha hoja ya msingi ya UFISADI wa kutisha kwenye uzinduzi wa Jiji,na swala la sisi kutomtambua MEYA.Ukweli ni kuwa Kamwe hatumtambui na hatutomtambua Meya kwa kuwa Hakuna uchaguzi wa meya uliowahi kufanyika Arusha.Huu ndio msimamo wangu na wa madiwani wenzangu wa chama chetu,na hakika tupo tayari kuufia huu msimamo.HATUMTAMBUI MEYA.Halimashauri imefika hapa kwa sababu ya MEYA tunayempinga kutokuwa na uwezo,nay eye kuwa sehemu ya ufisadi.Hivyo Meya wa kichina ni fisadi,pamoja na Mkurugenzi
1. .Mkurugenzi aeleze ilikuwaje kwenye kamati ya fedha apelike 66mil baraza 114,149,500mil,kwenye tamko lake la waandishi wa habari amesema 123,689,500mil,huu ni wizi na ufisadi mkubwa.
2. .Kwa nini hakuleta kwenye baraza michango ya 18mil ya AUWASA,12mil ya Jiangxi Geo Engeneering Group Corporation na 4mil ya China railway Seventh group?
3. Je kwa nini aliombea fedha kwenye swala ambalo tayari kuna wadau walishajitolea kuisadia Halimashauri?
“It is during our darkest moments that we must focus to see the light”
Imetolewa na
Nanyaro Ephata
…………………….
Diwani-Levolosi
18/11/2012
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO