Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Kesi za maandamano ya Chadema Arusha zashindwa kusikilizwa leo; washitakiwa 20 Usa River wafutiwa kesi

DSCN6291Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Arusha ambae pia ni Mwenyekiti wa Vijana wa Chama hicho Mkoa na Diwani wa Kata ya Levolosi ya Jijini Arusha, Mh Ephata Nanyaro akitoa ufafanuzi kwa wafuasi wa chama chake leo katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kuhusiana na kushindikana kusikilizwa kwa kesi zilizokuwa zinawakabili viongozi kadhaa wa chama hicho kufuatia maandamano na mgogoro mbalimbali ya kisiasa, baada ya majaji waliopangwa kusikiliza kutoonekana.

****
WAFUASI wa Chadema waliojitokeza Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kujua hatima ya kesi takriban tatu za muda mrefu zinazowakabili baadhi ya viongozi wa kitaifa wa chama hicho na wanachama wengine, wamejikuta wakirudi majumbani bila kufahamu hatima hiyo baada kushindwa kusikilizwa kwa kesi hizo kulikotokana na kinachohisiwa kuwa ni kutokuwepo kwa mawakili walipangiwa kusikiliza kesi hizo.

Kesi hizo zinajumuisha maandamano ya amani ya chama hicho ya Januari 5, 2011, mkesha wa wafuasi wa chama na viongozi wao katika Viwanja vya NCM ya zamani pamoja na mashitaka ya vijana waliokamatwa wakimsindikiza aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema kwenda ofisini kwake na baadae kuishia kuamua kukaa mahabusu Kisongo, mwishoni mwa mwaka jana.

Awali ilielezwa kuwa siku ya leo mawakili wawili walikuwa wamepangiwa na Mahakama Kuu Dar es Salaam kusikiliza mashauri hayo katika Mahakama Kuu Arusha, mashauri ambayo yalikuwa yamefunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na baadae kukatiwa rufaa na Wakili wa washitakiwa Bw Kimongolo Mahakama Kuu Dar es Dalaam kwa madai kuwa kesi zote zimekiuka Katiba ya nchi.

Miongoni mwa washitakiwa wakubwa katika kesi hizo ni pamoja na Mwenyekiti wa Chadema, Mh Freeman Mbowe, Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa, Mwanasheria machachari Mh Tundu Lissu.

Wengine ni Mh Godbless Lema na wanachama na baadhi ya viongozi wa chama Mkoa wa Arusha.

Mh Nanyaro alipotakiwa kueleza ni lini kesi hizo zitasikilizwa tena alieleza wasiwasi wa uwezekano wa kuahirishwa mpaka mwezi wa 4 mwakani kutokana na taratibu za mzunguko wa majaji kwa maana kwamba huwa wanapangiana awamu za miezi mitatu ambazo zinawezekana kuanza mwezi wa pili mwakani kwa ajili ya kuhudumia wananchi.

Walioshitakiwa kuharibu gari ya Kamishina wa Jeshi wafutiwa kesi

Katika hatua nyingine jumla ya washitakiwa 20 wafuasi, wanachama na viongozi wa Chadema waliokuwa wameshitakiwa kwa kudaiwa kuharibu gari la Kamishina wa Jeshi la Polisi, Isaya Mungulu siku ya uchaguzi wa marudio Arumeru Mashariki wako huru baada ya Mahakama kufuta kesi hiyo dhidi yao kwa kilichoelezwa kuwa ni kukosekana kwa ushahidi kwa upande wa Serikali.

Mwanzoni walikamatwa jumla ya watu 70, 50 wakatoka wakiwa Polisi na hao 20 wakabaki na kesi ya kujibu, ambayo leo imefutwa.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO