Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

KESI DHIDI YA MMILIKI WA HOTELI YA SNOWCREST YA JIJINI ARUSHA YAAHIRISHWA TENA

KESI ya madai inayomkabili mfanyabiashara ambaye pia ni mmiliki wa hoteli ya Snowcrest  ya Jijini Arusha, Bw Wilfred Tarimo imehairishwa tena juzi katika mahakama ya biashara kanda ya Arusha hadi desemba 14 mwaka huu mara baada ya upande wa mdaiwa kukataa kulipa kiasi cha fedha na riba anachodaiwa katika kesi hiyo.


Kesi hiyo nambari 9 ya mwaka 2012 mkurugenzi wa kampuni ya Grand Alliance Limited,James Ndika amefungua madai dhidi ya mmiliki wa hoteli ya Snowcrest Hotel and Wildlife Safaris Ltd ambaye ni Tarimo ambapo katika shauri hilo mdai analalamika kutapeliwa jumla ya kiasi cha $ 1.7 milioni sawa na sh,3 bilioni kwa ajili ya mauziano ya hoteli hiyo.


Katika kesi hiyo mlalamikaji anadai kwamba mmiliki huyo wa Snowcrest alimuuzia hoteli hiyo mnamo novemba mwaka 2011 na kumpatia hati mbili za eneo la hoteli hiyo lakini baadaye ilikuja kugundulika kwamba eneo la hoteli hiyo lina hati tatu .


Katika kesi hiyo mlalamikaji amedai kwamba hati moja kati ya hizo tatu ina mkopo wa kiasi cha sh,1.5 bilioni kupitia benki mojawapo hapa nchini ambapo mara baada ya kubainika ilikwamisha biashara ya mauziano ya hoteli hiyo.


Katika shauri hilo Ndika anaomba alipwe kiasi chote cha fedha alizotoa kwa ajili ya kuinunua hoteli hiyo sanjari na riba tangu siku ya mauziano kwa kuwa mmiliki wa hoteli hiyo alimdanganya na kumpatia hati mbili lakini kumbe badala yake ina hati tatu.


Mbele ya jaji anayesikiliza shauri hilo, Nyangarika alisema kwamba mara baada ya hatua ya usuluhishi kukwama katika kesi hiyo kufuatia upande wa mdaiwa kukataa kulipa kiasi hicho cha fedha na riba kwa mamlaka aliyonayo ameamua kuiharisha kesi hiyo hadi desemba 14 mwaka huu hadi pale mahakama itakapopanga tarehe ya kuanza kuisikiliza .


Mara baada ya jaji Nyangarika kutoa kauli hiyo aliwauliza mawakili wa pande zote mbili endapo wamekubalina na uamuzi wake na ndipo walipotamka kwa nyakati tofauti kwamba hawana pingamizi juu ya kauli hiyo na kisha kesi hiyo kuharishwa .


Katika kesi hiyo upande wa mlalamikaji unawakilishwa na wakili Melkizedeck Lutema huku upande wa mlalamikiwa unawakilishwa na wakili,Nelson Merinyo.

Imeandikwa na Woinde Shizza – Libeneke la Kaskazini Picha na www.easoko.com

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO