Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Kutoka Polisi Arusha: Watu 3 wanaosadikiwa kuwa majambazi wamefariki kabla ya kufikishwa Hospitali ya Mt Meru

Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Sabas akionyesha sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ0 ambazo zilikutwa  kwenye begi la watu watano ambao wanasadikiwa kuwa ni majambazi .Tukio hilo lililtokea katika eneo la Olmatejoo jijini Arusha leo asubuhi na Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwajeruhi kwa risasi Watatu kati yao ambao baadae walifariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitali

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Sabas akionyesha bunduki zilizokutwa kwenye begi la watu watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi ambapo watatu kati yao walijeruhiwa kwa risasi na askari wa jeshi la Polisi na kisha kufariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitali leo asubuhi

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Sabas akionyesha kitako cha bunduki aina ya Rifle iliyokutwa kwenye begi la watu watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi. Watatu kati yao walijeruhiwa kwa risasi na askari wa jeshi la polisi na kisha kufariki dunia leo asubuhi (Picha na Mahmoud Ahmad, Arusha KUPITIA Mjengwa Blog)

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO