Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Rest In Peace “Sharo Milionea”

Kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa na SULEIMANI MAGOMA BLOG inaelezwa kuwa Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga amethibitisha kwamba msanii wa muziki wa bongoflava na vile vile mchekeshaji maarufu kama Sharo Millionea amefariki dunia majira ya saa mbili za usiku wa jan Jumatatu tarehe 26/11/2012 kwa ajali ya gari eneo la Muheza, Tanga.

Rest In Peace Sharomillionea, kazi ya Mola haina makosa, umetangulia nasi tutafuata.

NOISE OF SILENCE BLOG  inaungana na ndugu,jamaa,marafiki na mashabiki wote wa Sharo Milionea katika msiba huu na kumuombea kwa Mungu apumzike mahali peama peponi.

Baadhi ya mastaa wengine wa Bongo ambao walifariki kutokana na ajali za barabarani ni pamoja na Mtoto wa Dandu, Mzee Issa Matona, baadhi ya waimbaji wa 5 Stars Morden Taarab akiwemo Issa Kijoti, na mchezaji wa Simba toka DRC, Mutesa Mafisango. Pia wako wasanii wengine wengi ambao wamenusurika ajlini akiwemo Roma Mkatoliki, Diamond na wengineo.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO