Mlipuko unaodhaniwa kutokana na bomu la kurushwa kwa mkono umetokea katikati ya ibada katika kanisa katoliki la Mt Joseph lililopo Olasiti Jijini Arusha ambako kwa siku ya elo kulikuwa na ibada ya Kuzindua Parokia ya Mt Joseph Olasiti.
Mlipuko huo unaelezwa kutokea majira ya katikati ya saa nne na saa tano asubuhi wakati Askofu wa Kanisa hilo akiendelea na ibada. Ibada hiyo sambamba na uzinduzi husika imeahirishwa hadi wakati mwingine.
Balozi wa Papa na ujumbe wake walikuwa miongoni mwa wageni muhimu katika tukio hilo la uzinduzi. Balozi huyo (tutakupatia jina lake baadae) alikuwa Arusha tangia alahamisi ya Mei 2, 2013 na alipatiwa ulinzi wa kutosha na Jeshi la Polisi.
Haijaweza kuthibitika hasa sababu za wahusika kurusha “bomu” lakini mmoja wa washukiwa tayari ametiwa nguvuni na Polisi.
Taarifa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa takribani watu wawili wanahisiwa kuwa wamefariki na makumi wengine kujeruhiwa vibaya na kukimbizwa hopsitali ya Mt Meru kwa matibabu.
Viongozi mbalimbali wa kijamii na kiserikali wameweza kufika eneo la tukio, miongoni mwao akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, Meya wa Manispaa ya Arusha, Gaudence Lyimo, na Mbunge wa Arusha Mjini Mh Gobless Lema.
Wengine ni Mbunge wa Arumeru Mashariki, mh Joshua Nassari, Diwani Msofe wa Kata ya daraja Mbili (CHADEMA), diwani wa Kata ya Olasiti na viongozi wengine wa Jeshi la Polisi na usalama Mkoa na Wilaya.
Jengo la kanisa halijadhurika lakini taharuki miongoni mwa watumiaji wa jengo hilo wakiwemo waumini wa kaisa hilo ni kubwa.
Chanzo cha mlipuko huo inasemekana kuwa kuna gari ndogo ilifika kanisani hapo na kusimama. Baadae alishuka mtu aliyekuwa amevalia vazi mithili ya kanzu na kurusha kitu kuelekea kanisani ambacho ndicho kilichosababisha mlipuko huo..
Lema hospitalini
Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema akiwa na mbunge wa Arumeru Joshua Nassari wametoa damu kwa ajili ya majeruhi walioumia katika mlipuko huo.
Lema amewahimiza wakazi wa Arusha na vijana kujitolea kwa wingi kuchangia damu ili kuokoa maisha ya majeruhi. Watu wengi wameitikia wito na wanaendelea kujitolea kuchangia damu kama ishara ya kumuunga mkono mbunge wao.
Hali ya eneo mlipuko ulipotokea
Waumini na wananchi wengine wakiwa na shauku ya kujua kilichotokea
Viongozi wa Kanisa wakitoa taarifa ya kilichotokea kwa waandishi wa habari kabla ya Balozi wa Papa kuondolewa Kanisani hapo chini ya ulinzi mkali wa Polisi.
Wanasualama Mkoa wa Arusha, wakijadiliana jambo katika eneo la tukio
Meya wa Manispaa ya Arusha, Mh gaundence Lyimo akielekea eneo la tukio kwa miguu baada ya utaratibu wa kutumia magari kuwa mgumu kutokana na idadi kubwa ya watu na magari yaliyoziba njia.
Magesa Mulongo akiteta na RCO wa Mkoa wa Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, magesa Mulongo akijiandaa kuzungumza na wananchi kanisani hapo na kuahidi kuwa Serikali itahakikisha watu wote waliohusika na jaribio hilo ovu, pamoja na mtandao wao wanakamatwa. Alidai pia vikosi vya Jeshi maalumu kwa kuchunguza milipuko vitafika eneo hilo ili kufanya uchunguzi. Taarifa za eneo la tukio zinaeleza kuwa tayari kuna mshukiwa mmoja ameshatiwa mbaroni na yuko mikononi mwa Jeshi la Polisi kwa mahojiano na uchunguzi zaidi.
Eneo lenye utepe ndipo kitu hicho kinachodhaniwa kuwa bomu kilipoangukia. Pichani unaweza kuona wigi za kichwani na viatu vya waumini vikiwa vimesambaa baada ya wenyewe kuviacha, miongoni mwao wakiwa ni majeruhi.
Balozi wa Papa akisindikizwa na ulinzi mkalai kutoka kanisani hapo
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo akizungumza na mmoja wa mapadri wa Kanisa hilo kupewa maelezo ya kuhusu kilichotokea kanisani hapo.
Watoto waliopotezana na ndugu zao
KWA PICHA ZA MAJERUHI NA MATUKIO MENGINE ZITAKUJIA BAADAE KIDOGO HAHA HAPA ARUSHA255 BLOG
0 maoni:
Post a Comment