Taarifa ambazo Blog hii imezipata hivi punde zinaeleza kuwa mlipuko mkubwa umetokea Jijini Arusha katika Kanisa Katoliki lililopo eneo la Olasiti.
Inaelezwa kuwa leo kulikuwa na Ibada ya kuzindua Parokia ya Mt Joseph Olasiti ambapo Balozi wa Papa alikuwa miongoni mwa wageni.
Mlipuko huo unahisiwa kutokana nakinachohisiwa kuwa bomu la kurusha kwa mkono ambalo linadaiwa kurushwa na mtu aliyepita jirani na Kanisa hilo.
Tunaendelea kufuatilia taarifa zaidi kujua hali ilivyojiri na tutakujuza hapa hapa muda mfupi ujao…
Ulinzi ukiimarishwa eneo ulipotokea mlipuko huo na kujeruhi makumi ya waumini
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, magesa Mulongo akipata maelezo toka kwa padri wa kanisa la Mt Joseph Olasiti ambapo mlipuko huo umetokea..
1 maoni:
kweli ni uhasama huu.......ndio tuseme visa vya Zanzibar ndio vimefika Arusha? Mungu wape nguvu majeruhi wote. Wewe shetani hauwezi shinda.
Post a Comment