Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MAADHIMISHO YA SIKU YA VYOMBO VYA HABARI AFRIKA MASHARIKI YAFANA JIJINI ARUSHA; KATIBU MKUU EAC ATAKA UHURU WA HABARI ULINDWE

Mratibu wa Media Center kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC)Florian Mutabuzi(kushoto)akisalimiana Mwenyekiti wa APC,Claud Gwandu huku Mkuu wa mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo na Rais UTPC,Kenneth simbeye wakishuhudia 

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC)Dk Richard Sezibera akizungumza katika maadhimisho

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC)Dk Richard Sezibera akiwa amempakata Moria,mtoto wa hayati Daudi Mwangosi aliyeuawa na mkoani Iringa,kushoto ni mjane wa Mwangosi

Rais wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari nchini(UTPC)Aboubakar Kasan(kushoto)akiwa na mjane wa daudi Mwangosi

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC)Dk Richard Sezibera(katikati)na Mkurugenzi wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari nchini(UTPC)Aboubakar Kasam(Kulia) wakimkabidhi hundi yenye thamani ya Sh 5 milioni mjane wa marehemu Daudi Mwangosi

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC)Richard Owora akibadilishana mawazo viongozi mbalimbali wa tasnia ya habari nchini

Wadau wa sekta ya habari kutoka shoto ni Claud Gwandu,Rais wa UTPC,Kenneth Simbeye na Mjumbe wa MCT,Allan Lawa

 

Waandishi wa habari wakongwe wakijadili jambo

Mkuu wa mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo(shoto)Balozi wa Sweden nchini Lennarth Hjelmaker na Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Nyirembe Munasa wakifurahia jambo

Mkuu wa mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo(shoto)akifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Deus Kibamba na Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Nyirembe Munasa wakifurahia jambo

Mwandishi wa habari wa The Citizen mkoa wa Arusha,Zephania Ubwani(shoto)Makwaiya wa Kuhenga wakisalimiana

Waandishi wakongwe

Waandishi wakifatilia mada

Wadau wa habari wakifatilia kwa makini

Dk Sezibera akihutubia

Burudani iliyowatoa wajumbe machozi

PICHA ZOTE NA FIBERT RWEYEMAMU

***********************************

Nae Ramadhani Siwayombe, wa Tanzania Daima Arusha anaripoti zaidi….

Sezibera: Uhuru wa habari lazima ulindwe

KATIBU Mkuu wa Jumuia ya Afrika Mashariki, Balozi Richard Sezibera amesema uhuru wa kupata na kutoa habari katika taifa lolote ni sehemu ya uwazi wa utendaji wa viongozi wa serikali na taasisi.

Balozi Sezibera alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua rasmi mkutano wa siku mbili wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani inayoadhimishwa kitaifa mkoani Arusha.

Alisema kuwa uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kupata habari vyote kwa pamoja vinahitajika kulindwa kwa ajili ya maendeleo ya umma.

Alisema uhuru wa vyombo vya habari si kitu kigeni kwani unatokana na mikataba ya kimataifa ambapo miongoni mwake umo huo wa uhuru wa vyombo vya habari ambao mataifa mengi yameusaini na kuuridhia.

Sezibera licha ya kusisitiza kulindwa kwa uhuru huo wa vyombo vya habari, pia aliviasa vyombo hivyo vya Afrika kuanza kuandika habari nzuri za maendeleo yanayopatikana katika nchi hizo.

Alisema kwa Bara la Afrika miaka 10 nyuma hali ilikuwa ngumu kiuchumi wakati ule wa ubanaji matumizi, lakini sasa hali imebadilika na kuwa nzuri, hivyo ni jukumu la vyombo hivyo kuandika mafanikio hayo.

Aliongeza kuwa anasikitishwa anaposoma magazeti ya nchi hizo za Kiafrika na kukuta habari za Afrika zilizonukuliwa kutoka mashirikia ya habari ya nje ya bara.

“Inakuwaje waandishi wetu na vyombo vyetu vya nyumbani kunukuu habari za ndani kutoka CNN badala ya habari hizo kuandikwa na sisi wenyewe tulio katika maeneo husika halafu CNN wakaipata habari kupitia vyombo vyetu?” alihoji.

Sezibera alitoa pole kwa wanahabari wote Afrika Mashariki kutokana na vifo na madhara mbalimbali ambayo wamepata wanahabari kwa kipindi chote cha kutimiza majukumu yao.

Katika hatua nyingine, katibu mkuu huyo, alimkabidhi hundi ya cheki ya sh milioni 5 mjane wa marehemu Daudi Mwangosi,  aliyeuawa kwa bomu na polisi mkoani Iringa, iliyotolewa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).

Awali, akimkaribisha Balozi Sezibera, mwanasheria Mohamedi Tibanyendelea alielezea umuhimu wa siku ya uhuru wa vyombo vya habari akisema katika siku mbili za mkutano huo mada mbalimbali zitatolewa.

Alisema kuwa mada kuu ni usalama na mazingira bora ya utendaji kwa mwandishi wa habari.

Mada nyingine ni mabadiliko ya vyombo vya habari ikihusisha pia maslahi ya mwandishi kisha kutakuwa na azimio ambalo litajumuisha yote yaliyojadiliwa ambalo litaitwa Azimio la Arusha.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO