Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

News Updates: Mahakama ya Rufaa yatupilia mbali pingamizi dhidi ya rufaa ya Lema, kesi ya msingi itaendelea

Pingamizi lililowekwa na upande wa wajibu rufani kupitia Wakili wao Alute Mughwai  ili rufaa ya Lema kupinga kuvuliwa ubunge isisikilizwe limetupiliwa mbali na Mahakama ya Rufaa baada ya kuridhika kwamba kosoro zilizolalamikiwa zilikuwa kwa upande wa Mahakama.
Pia kifungu kilichomhukumu Lema kina maksoa hivyo kesi itatajwa tena baada ya siku 14 kwa ajili ya kuendelea kusikiliza hoja za walio kata rufaa.
Mawakili wa Mh Godbless Lema wanahitajika kutimiza mahitaji fulani ya kisheria ndani ya siku 14 ili shauri la rufaa hiyo iweze kupangiwa siku ya kusikilizwa na kuamuliwa.
Wadaiwa kwenye shauri hilo ni wanachama watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mkanga, Agness Mollel na Happy Kivuyo, waliofungua shauri lililotengua ubunge wa Lema wakidai kuwa wakati wa kampeni alimdhalilisha mgombea wa CCM, Dk. Batilda Burian kwa kutumia lugha za matu
Lema anawakilishwa na Wakili Method Kimomogoro, anayesaidiana na Tindu Lissu.
IMG-20121108-WA0007
IMG-20121108-WA0006
Baadhi ya wananchi, wapenzi wa Chadema wakimlaki Mh Lema mara baada ya kuwasili katika viwanja vya mahakama.
IMG-20121108-WA0004
Jopo la Majaji likiwa tayari kuanza kazi
IMG-20121108-WA0003Kutoka kushoto, Henry Kileo, Nuru Ndosi na Mh Godbless Lema
IMG-20121108-WA0002Henry Kileo akiwa ndani ya ukumbi wa Mahakama Kuu, Dar es Salaam
IMG-20121108-WA0005Katibu wa Chadema Kanda ya Kinondoni, Henry Kileo (kushoto) akibadilishana mawazo na mdau wa Chadema mara baada ya kuwasili viwanja vya Mahakama Kuu
IMG-20121108-WA0008
IMG-20121108-WA0009
Wananchi na viongozi wakiingia kuandikisha chumba cha mapokezi katika Ofisi ya Chadema Kinondoni, Dar es Salaam.
IMG-20121108-WA0010Picha tatu za mwisho, baada ya shauri kuamuliwa, Mh Lema akiwashukuru wananchi waliojitokeza katika ya ofisi ya Chadema  Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 maoni:

Mr Kiwelu. said...

Hongera Lema, Chadema ni noma hawatuwezi, ng'o!

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO