Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA: KIKWETE AKIZINDUA TAASISI SAYANSI NA TEKNOLOJIA YA CHUO KIKUU CHA NELSON MANDELA ARUSHA JANA

Rais Jakaya Kikwete, akikata utepe kuweka jiwe la Msingi ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo Kikuu cha Nelson Mandera, jijini Arusha, Novemba 2, 2012. Kushoto kwake ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Chuo hicho, Dk. Mohammed Gharib Bilal. Kushoto ni Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Burton Mwamila.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandera, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo Kikuu cha Nelson Mandera, jijini Arusha , Novemba 2, 2012. Kulia ni Rais Jakaya Kikwete, aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo.

Rais Jakaya Kikwete, akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo Kikuu cha Nelson Mandera, jijini Arusha, Novemba 2, 2012. Kulia kwake ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Chuo hicho, Dk. DMohammed Gharib Bilal. Kulia ni Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Burton Mwamila.

Rais Jakaya Kikwete, akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Makamu wake na Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandera, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Burton Mwamila, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo Kikuu cha Nelson Mandera, jijini Arusha
HABARI NA PICHA ZOTE NI KWA HISANI YA JAMII BLOG (PAMELA MOLLEL)Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO