Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

2015: URAIS WA DAMU.; GENGE HATARI LAIBUKA, CCM, CHADEMA VYAHUSISHWA.

Dk Steven Ulimboka akiwa chumba cha wagonjwa mahututi MOI.

Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Limited, Absalom Kibanda, akiwa ndani ya Ndege ya Flightlink

Daudi Mwangosi aliyekuwa mwandishi wa chanel ten akisulubiwa na askari polisi na kumfyatulia bomu la machozi mwilini na kupoteza maisha mkoani Iringa.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Hali halisi publishers Ltd, Saed Kubenea akiwa katika wodi ya Hospitali ya Apollo, New Delhinchi INDIA mara baada ya kufanyiwa Upasuaji macho, Kubenea amekuwa akitibiwa katika Hospitali hiyo tokea mwaka 2008 alipomwagiwa tindikali katika ofisi yake jijini Dar es Salaam na hii ni operesheni yake ya tano.

**********

SASA ni dhahiri kwamba, makundi yanayohasimiana ndani ya vyama vikuu vya siasa kwa sababu ya kusaka ukuu wa dola mwaka 2015, yako tayari kufanya jambo lolote kuhakikisha yanafanikisha malengo ya kuupata urais baada ya rais wa sasa, Jakaya Kikwete, kumaliza muda wake, MTANZANIA Jumatano linaripoti.

Mlolongo wa matukio ya utekaji, utesaji na mauaji ya watu maarufu hapa nchini ambayo yamekuwa yakihusishwa na makundi ya watu wanaousaka urais, ni ushahidi tosha kwamba, makundi hayo yako tayari kuingia Ikulu si kwa kutumia nguvu ya fedha tu, bali hata kwa kufanya jambo lolote ambalo litahakikisha ushindi wao.

Wachambuzi na wafuatiliaji wa masuala ya kisiasa wa hapa nchini wanayatafsiri matukio ya sasa ya uhalifu dhidi ya binadamu kuwa ni mkakati unaoratibiwa kwa karibu na makundi yanayowania urais mwaka 2015 ndani na nje ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kwamba, ndani na nje ya CCM, vita ya kisiasa baina ya makundi hasimu imekuwa kubwa kwa kiwango cha baadhi ya wanasiasa kuwa na fikra za kuangamizana na ama kupeana vilema vya maisha, ili kutimiza ndoto ya kuukwaa urais.

Kwa upande mwingine, nje ya CCM, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambacho kwa muda mrefu kimekuwa kikinyooshewa kidole na CCM kwa kuendesha siasa za kibabe zinazogharimu maisha ya Watanzania, nacho sasa kinakabiliwa na vita ya makundi yanayowindana kuwania urais mwaka 2015. 

Ni mwenendo huo wa siasa za ndani uliosababisha mgawanyiko kwa wafanyakazi wa Idara ya Usalama wa Taifa, ambako uchunguzi unaonyesha kuwa baadhi yao wameasi na kuamua kufanya kazi kwa karibu na makundi yanayowania urais, badala ya ile ya kusimamia maslahi ya taifa.

Vyanzo vya habari kutoka ndani ya makundi hayo, vinaeleza kuwa matukio ya sasa ya kudhuru watu maarufu yanadaiwa kufanywa na watumishi wenye mafunzo ya kutesa na kuua walio ndani ya Idara ya Usalama wa Taifa kwa malengo yenye maslahi fulani fulani.

Mmoja wa wanasiasa maarufu hapa nchini ambaye amepata kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, amelieleza MTANZANIA Jumatano kuwa vitendo vya kushambulia na kudhuru raia vinafanywa na watumishi wa Idara ya Usalama walioviasisi kwa madhumuni ya kuwachonganisha wananchi na serikali yao, ili wazidi kujenga chuki na watawala.

Anaeleza zaidi kuwa wanausalama wanaodaiwa kuasi kutokana na kukatishwa tamaa na mwenendo wa uendeshaji serikali sasa wamejipenyeza na kuwa wakala wa moja ya kundi la wanaCCM linalopambana na makundi mengine ya ndani ya chama hicho kushika ukuu wa dola na wapo pia wanaodaiwa kujipenyeza katika vyama vya upinzani, hususani Chadema na kushiriki harakati za kuiondoa CCM madarakani. 

Habari zinadai kuwa ndani ya CCM wanausalama waasi wamekuwa wakitumiwa na baadhi ya makundi hayo kutekeleza azma yao, ikiwa ni pamoja na kutekeleza mpango wa kuumiza watu wenye ushawishi kwa jamii ambao mwenendo wao una athari mbaya kwa makundi hayo.

Mkakati unaotajwa wa kuwatumia waasi hao ni kuhakikisha wanadhoofisha makundi mengine ambayo ni kikwazo kwao kwa staili ya kutoa vitisho, kupanga mipango ya kuteka watu na kujeruhi.

Duru za habari zimeeleza kuwa hatua ya Chadema kudaiwa kuhusika katika mipango ya utekaji na utesaji wa watu mbalimbali, wakiwemo waandishi wa habari, ni mkakati unaoratibiwa na maofisa usalama wa taifa walioasi, wanaotumiwa sasa na wapinzani na baadhi ya makundi ya wanaCCM.

Kwamba mkakati huo, unaratibiwa kwa malengo mawili tofauti, la kwanza likitajwa kuwa ama Chadema wanashirikiana na watu hao kupanga vitendo hivyo ili kujenga chuki baina ya serikali iliyoko madarakani na wananchi au kundi la wanaCCM linalopambana chini ya kivuli cha kuilinda serikali, lakini likiwa na nia ya kuichafua ili kufanikisha lengo lake la kushika dola.

Hoja hii inajengwa na wafuatiliaji wa mambo katika msingi kwamba endapo vyombo vya ulinzi na usalama visingebaini mipango hiyo, maana yake ni kwamba tukio ambalo lingetokea moja kwa moja lingeihusisha serikali ambayo nayo imekuwa ikinyooshewa vidole, ikidaiwa kuhusika na matukio ya utekaji na utesaji wa watu maarufu kama ilivyotokea kwa kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka.

Taarifa za kikachero zilizokusanywa na MTANZANIA Jumatano, zimeeleza kuwa ingawa hadi sasa utekelezaji wa mpango wa kumteka na kumtesa Dk. Ulimboka, uliratibiwa kiufundi na watu wenye taaluma ya kikachero, walitumia mwanya wa mgomo wa madaktari kukoleza chuki ya wananchi dhidi ya serikali na kwamba hata waliofichua uhusika wa mmoja wa maofisa wa Ikulu katika sakata hilo walikuwa na malengo hayo hayo. 

Kwa upande mwingine, wafuatiliaji wa siasa za mataifa mbalimbali wanasema tukio la vyama vya upinzani, hususani Chadema kuhusishwa na matukio ya kigaidi huenda ikawa chama hicho, katika kuhakikisha kinaingia Ikulu, kimeamua kutumia siasa za staili ya watu wa aina ya Apollo Militon Obote wa Uganda.

Obote, rais wa zamani wa Uganda, wakati fulani alipoondolewa madarakani chama chake kilishutumiwa kufanya vitendo vya kigaidi dhidi ya wananchi ili kuwafanya wajenge taswira mbaya dhidi ya serikali yao.

Vivyo hivyo inaelezwa kuwa wakati wa utawala wa Iddi Amin nchini Uganda, ambao ulikuwa ukishutumiwa kwa vitendo vya kinyama, si vyote vilikuwa vikifanywa na serikali yake, bali inadaiwa kuwa makundi ya misituni yaliyokuwa yakipigana kuingia madarakani kama yale ya akina Yoweri Museveni, nayo yalishiriki katika vitendo hivyo, lakini wao hawakuonekana. 

Ni kwa namna hiyo hiyo, matukio ya mauaji ya mwandishi wa habari wa kituo cha Channel Ten, Daudi Mwangosi na hata kuvamiwa kwa Ofisi za Gazeti la Mwanahalisi na kujeruhiwa kwa wahariri wake wawili kunaelezwa kuwa unaweza kuwa mpango mahususi wa kundi la wanausalama lililoasi huku likiwa ndani ya serikali kuichafua Ikulu.

Tukio jingine ambalo linaangaliwa kwa mtizamo huo ni kutekwa na kuteswa vibaya kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda, anayeaminika kuwa na nguvu ya ushawishi miongoni mwa wanahabari ambaye aina ya kuteswa kwake inafanana kwa kiwango kikubwa na ile ya Dk. Ulimboka.

Katika mwendelezo huo huo wa matukio ya aina hiyo, kuuawa kwa viongozi wa dini, mgogoro wa kidini wa kuchinja nyama na hata uchomaji moto nyumba za ibada ni vitendo vinavyodaiwa kutekelezwa makusudi na kundi hilo, lengo likiwa kuamsha hasira za wananchi dhidi ya serikali.

Hata hivyo, ni Chadema ambacho sasa kinaonekana kuwa katika wakati mgumu zaidi wa kujinasua na doa la kuhusishwa na vitendo vya utekaji na utesaji raia kutokana na mfululizo wa tuhuma za aina hiyo ambazo kimekuwa kikielekezewa.

Madai haya yanapewa nguvu na malalamiko yaliyopata kutolewa na Naibu Katibu Mkuu wake, Zitto Kabwe, ambaye mwishoni mwa mwaka jana akiwa katika mkutano wa kawaida wa viongozi wa chama hicho, alishutumiwa vikali na viongozi wenzake kwa kukivuruga Chadema na katika kile kinachoonekana kuumizwa na tuhuma hizo, Zitto alifunua siri ya mpango wa kumuua aliodai kuandaliwa na viongozi wenzake.

Sambamba na madai haya ya Zitto, jambo jingine ambalo limekuwa likikitesa Chadema ni tuhuma za kupanga mauaji ya aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe, ambaye harakati zake za kisiasa ndani ya chama hicho na hasa nia yake ya kuwania uenyekiti ilielezwa kuwa moja ya sababu za kutekelezwa kwa mauaji yake.

Chanzo: http://www.mtanzania.co.tz picha na mitandao

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO