Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Hospitali ya Mt Meru Yapatiwa Msaada wa Mablanketi 100 na Mbunge Catherine Magige, Viti Maalum CCM kupitia vijana

Mbunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Viti Maalum CCM, Mh Catherine Magige ambaye amepitia kundi la vijana, UVCCM ametoa msaada wa mablanketi mia moja, sabuni hospitali ya Mt Meru ya Jijini Arusha.

Magige ambaye ubunge wake umetokana na leseni ya UVCCM Jijini hapa, pia ametembelea wagonjwa katika hopsitali hiyo na vituo vituo viwili vya watoto yatima na kuwapa zawadi ya chakula cha Pasaka pamoja na vinywaji.

Mwaka jana, Mh Magige alikwenda Hospitali hapo na kuwapa zawadi wagonjwa takriban 125.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Catherine Magige, akimkabidhi
mmoja wa wazazi blanketi alipotembelea wadi ya wazazi leo kwenye Hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mt. Meru

 

 

 

Mbunge wa Viti Maalum,kupitia UVCCM (CCM) mkoani Arusha Bi. Catherine Magige ambaye ni Kiongozi wa Taasisi ya Catherine Foundation, akimkabidhi Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru, Frida Mokit msaada wa mablang’eti ya kujifunikia wagonjwa waliolazwa Hospitalini hapo.

Taasisi ya Maendeleo isiyo ya kiserikali ya Catherine Foundation ya jijini Arusha Machi,28,2013 imetoa misaada mbalimbali ya vyakula kwa wagonjwa Hospitali ya Mt Meru na vituo viwili vya Yatima vya Faraja na Lohada Moshono vyote vya jijini humo.

Mbunge wa Viti Maalum wa UVCCM (CCM), Catherine Magige ambaye ni Kiongozi wa Taasisi ya Catherine Foundation, akiwajulia hali wagonjwa waliolazwa Hospitali ya Mt. Meru ya jijini Arusha na kuwapa zawadi mbalimbali.

Misaada hiyo ya vyakula na sabuni pamoja na kuwatembelea wagonjwa kufanyika ikiwa ni sehemu ya kuwapa faraja wagonjwa na yatima hao wakati huu wa kuelekea sikukuu ya Pasaka ili nawao wajisikie ni miongoni mwa jamii.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO