Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Papa Francis atawazwa rasmi

 

Sherehe za kumtawaza kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, zimefanyika katika viunga vya Kanisa la Mtakatifu Petro mjini Roma, ikiwa ni ishara ya kuanza rasmi kwa shughuli zake za Papa.

Mapema, Papa Francis alizunguka katika viunga hivyo akiwa katika gari la wazi, akiteremka kuwabariki mahujaji waliofika hapo.

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki, amewataka viongozi na watu wote duniani kuwalinda wanyonge na watu maskini. Watu wapatao laki mbili (200,000) wamehudhuria sherehe hizo.

Papa Francis alichaguliwa na mkutano wa Makadinali wiki iliyopita kuchukua nafasi ya Papa Benedict XVI aliyetangaza kujiuzulu wadhifa huo tarehe 28 Februari 2013.

Papa Benedict amekuwa papa wa kwanza kujiuzulu katika miaka 600 ya historia ya Kanisa Katoliki. Alitangaza kujiuzulu mwezi uliopita akitaja sababu za umri wake wa miaka 85 na kwamba asingeweza kutekeleza kikamilifu majukumu yake.

Papa huyo wa kwanza kutoka bara la Amerika, anaonekana kuwa na mtazamo tofauti na watangulizi wake.

BBC Swahili

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO