Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Serengeti bia yazindua Kampeni kabambe

 

Mkurugenzi wa Masoko SBL Ephrahim MafuruKampuni ya bia ya Serengeti (SBL)imezindua kampeni yake mpya ya kinywaji cha bia ya Serengeti kampeni itakayofanyika nchi nzima lengo likiwa kuitangaza bidhaa pia kushiriki mafanikio inayopata pamoja na watanzania.

Mkurugenzi wa Masoko SBL Ephrahim Mafuru akizindua kampeni hiyo mbele ya waandishi wa habari alisema kampini hiyo imepewa jina la tupo pamoja katika shangwe za mafanikio na kuongeza kuwa itaanza mapema wiki hii.

"Hii ni kampeni ambayo haijawahi kutokea, unajua SBL imekuwa ikipata faida hivyo lazima tutumie faida hiyo katika kuwanufaisha watanzania, katika kampeni yetu hii kuna zawadi mbalimbali tutakuwa tukizitoa,"alisema Mafuru

Alisema kampeni hiyo itakayokuwa ikiuliza Shangwe itakuwa wapi itaendeshwa katika mikoa yote nchini na kwamba wafanyakazi wamejipanga katikakuhakikisha kuwa kampeni hiyo inafanya vizuri.

Alisema bia ya Serengeti ambayo imeendelea kuwa bora zaidi hapa nchini wataendelea kuitangaza pia kushiriki shughuli za maendeleo pale wanapopata nafasi na wanapopata faidi kwa lengo la kuinua uchumi wa taifa hili.

Credit: HabariMpya.Com

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO