Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

SIMBA YAPIGWA 4-0+1-0, AZAM YAUA 5-0+3-1; AZAM KUCHEZA NA TIMU YA GEORGE WEAH AFRIKA


KAMA ilivyotarajiwa na wengi, Azam ndio timu pekee iliyobaki kwenye michuano ya Afrika, baada ya jioni ya jana kuifunga Al Nasir ya Juba, mabao 5-0 kwenye Uwanja wa Juba, Sudan Kusini.

Kwa matokeo hayo, Azam inaingia Raundi ya Pili ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa ushindi wa jumla wa mabao 8-1, kufuatia ushindi 3-1 katika mchezo wa kwanza wiki mbili zilizopita Dar es Salaam.

Katika mchezo huo, mabao ya Azam yalifungwa na Kipre Herman Tchetche, John Raphael Bocco kila mmoja mawili, moja kila kipindi na lingine Khamis Mcha ‘Vialli’.

Mapema jioni ya jana, Jamhuri ya Pemba, ilikuwa timu ya kwanza ya Tanzania kuaga michuano ya Afrika, baada ya kufungwa mabao 5-0 na wenyeji Kedus Giorgis nchini Ethiopia katika mchezo wa marudiano, Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika.

Matokeo hayao, yanamaanisha, Jamhuri imeaga kwa kufungwa jumla ya mabao 8-0, baada ya awali kutandikwa 3-0 katika mchezo wa kwanza Uwanja wa Gombani, Pemba.

Wawakilishi wengine wa Bara katika michuano hiyo, Simba SC wametolewa baada ya kufungwa mabao 4-0 na Recreativo de Libolo ya Angola kwenye Uwanja wa Manispaa mjini Calulo, Angola.

Matokeo hayo, yanaifanya Simba itolewe kwa jumla ya mabao 5-0, baada ya awali kufungwa bao 1-0 Dar es Salaam.

Hadi mapumziko, Libolo walikuwa mbele kwa bao 1-0, lakini kipindi cha pili ndipo hali ikawa mbaya zaidi kwa Wekundu wa Msimbazi baada ya kutandikwa mabao hayo matatu na kuwa 4-0.

Simba ilicheza vizuri kipindi cha kwanza, lakini Recreativo walitumia zaidi upande wa kushoto kushambulia, ambako walimzidi beki Amir Maftah na kumgeuza uchochoro.

Na hata bao hilo la kwanza lilitokana na Maftah kuzembea kuokoa mpira hadi mfungaji akaingiza mguu kutokea nyuma yake na kufunga.

Kipindi cha pili, Simba ilifanya mabadiliko, ikiwatoa Amir Maftah na kumuingiza Kiggi Makassy kwenda kucheza beki ya kushoto, wakati Mrisho Ngassa alikwenda kuchukua nafasi ya Chanongo.

Mabadiliko hayo hayakuisaidia Simba SC, kwani Kiggi alikwenda kuwa uchochoro zaidi kuliko Maftah na Libolo wakapitia huko kutengeneza mabao yao, waliyoyapata dakika 15 za mwishoni.

Hata mabeki wa kati nao, waliwaruhusu wachezaji wa Angola kuruka peke yao kwenye mipira mingi ya juu, hivyo kufunga kwa urahisi.

Kikosi cha Simba kilikuwa; Abbel Dhaira, Nassor

Massoud ‘Chollo’, Amir Maftah/Kiggi Makassy, Komabil Keita, Juma Nyosso, Shomary Kapombe, Amri Kiemba, Abdallah Seseme, Haroun Chanongo/Mrisho Ngasa, Felix Sunzu na Salim Kinje.

AZAM KUCHEZA NA TIMU YA GEORGE WEAH AFRIKA

Na Princess Asia

AZAM FC, sasa itamenyana na Barrack Young Controllers II ya Liberia, nchi anayotoka mwanasoka pekee wa Afrika kuwahi kushinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Ulaya na Dunia, George Opong Weah katika Raundi ya Pili ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, kufuatia jana kuitoa Al Nasir Juba ya Sudan Kusini.

Azam jana imeitoa Al Nasir, kufuatia ushindi wa ugenini wa mabao 5-0, ambao unafanya ushindi wake wa jumla uwe 8-1, baada ya awali kushinda 3-1 Dar es Salaam.

Barrack Young Controllers II nayo imeifunga Johansens ya Sierra Leon bao 1-0 ugenini kufuatia sare ya bila kufungana katika mchezo wa awali ugenini.

Kama ilivyotarajiwa na wengi, Azam ndio timu pekee iliyobaki kwenye michuano ya Afrika, baada ya jana kuitoa Al Nasir ya Juba.

Katika mchezo huo, mabao ya Azam yalifungwa na Kipre Herman Tchetche, John Raphael Bocco kila mmoja mawili, moja kila kipindi na lingine Khamis Mcha ‘Vialli’.

Jamhuri ya Pemba, ilikuwa timu ya kwanza ya Tanzania kuaga michuano ya Afrika, baada ya jana jioni kufungwa mabao 5-0 na wenyeji Kedus Giorgis nchini Ethiopia katika mchezo wa marudiano, Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika.

Matokeo hayo, yanamaanisha, Jamhuri imeaga kwa kufungwa jumla ya mabao 8-0, baada ya awali kutandikwa 3-0 katika mchezo wa kwanza Uwanja wa Gombani, Pemba.

Wawakilishi wengine wa Bara katika michuano hiyo, Simba SC wametolewa pia baada ya kufungwa mabao 4-0 na Recreativo de Libolo ya Angola kwenye Uwanja wa Manispaa mjini Calulo, Angola.

Matokeo hayo, yanaifanya Simba itolewe kwa jumla ya mabao 5-0, baada ya awali kufungwa bao 1-0 Dar es Salaam.

Azam wataanzia ugenini mechi ya kwanza, kati ya Machi 15 na 17, mwaka huu kabla ya kurudiana wiki mbili baadaye na wakivuka mtihani huo watakutana na mshindi kati ya FAR Rabat ya Morocco na Al Nasr ya Libya.

Taarifa na BIN ZUBEIRY BLOG

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO