Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

CCM kuiiga CPC kuinua vijana

na Mwandishi maalum, Chengdu, China

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, amesema chama hicho kitaihimiza serikali yake kuiga mbinu zinazotumiwa na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ya kuweka vituo vya vijana wajasiriamali wasomi, kuwezesha wanaomaliza elimu ya juu, ili waweze kutumia vipaji vyao kujiajiri badala ya kusubiri kuajiriwa.

Kinana alisema hayo juzi baada ya yeye na ujumbe wake wa watu 14 waliopo katika ziara ya siku 10 ya mafunzo nchini China kutembelea kituo cha vijana wajasiriamali cha Chengdu, Jimbo la Sichuan na kushuhudia jinsi vijana wasomi walivyoweza kutumia vipaji vyao kujiajiri.

“Kwa kweli vijana hawa wanaonesha umahiri mkubwa wa kutumia vipaji vyao, ni muhimu nasi tukaiga namna hii bora ya kuwaweka vijana pamoja, kwa sababu inasaidia kupunguza tatizo la ajira, pia kuleta faida kwa taifa,” alisema Kinana.

Kinana alimwagiza Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Martine Shigela, aliyeko kwenye msafara wake, kuwasiliana na uongozi wa kituo hicho ili kuona namna mbinu zinazotumika kuwakusanya vijana kwenye kituo hicho zitakavyoweza kufanyika Tanzania.

Katika ziara hiyo, Kinana na msafara wake walivutiwa baada ya kushuhudia vijana wanavyobuni na kutengeneza vifaa vya kielektroniki kama vya simu, redio, televisheni na wengine kubuni katuni, michezo na manjonjo mbalimbali ambayo huwekwa katika kompyuta na simu za mkononi kwa ajili ya wenye vifaa hivyo kujiliwaza.

Akizungumza wakati akitoa maelezo kuhusiana na kituo hicho, Mkuu wa kituo hicho, Zheng Xiola, alisema vijana zaidi ya 100 wameweza kukusanywa kwenye kituo hicho kwa ajili ya kufanya kazi mbalimbali za ubunifu katika mambo ya teknolojia hasa kuhusu elektroniki.

Alisema wakati wapo wanaobuni na kutengeneza vifaa vya kielektroniki kama vya simu, redio, televisheni na vifaa vingine vinavyotumia umeme, wengine ni wabunifu na watengenezaji wa vikatuni, michezo na manjonjo mbalimbali kwa ajili ya kompyuta au simu.

Xiola alisema kazi hizo zimewafanya vijana wengi wanaomaliza masomo ya elimu ya juu kujiari kwa njia hiyo, kwa kuwa kazi zao huuzwa ambapo kwa wale wanaotengeneza katuni, michezo na manjonjo ya kwenye simu au kompyuta huweza kuuza kwa kampuni zinazotengeneza vifaa hivyo na wanaotengeneza vifaa vya kielektroniki huweza kuuzia.

1B

KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipata maelezo kuhusu shughuli za  kilimo alipotembelea mji wa Dantong, Nanchong kwenye miradi ya kilimo kwa ajili ya kupambana na umasikini, Machi 16, 2013. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai. Kinana yupo nchini China na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya nyanja mbalimbali za kimaendeleo, kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha nchi hiyo cha CPC.

Chanzo: Tanzania Daima, Picha na Bashir Nkoromo

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO