Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mgomo wa Daladala Jijini Arusha asubuhi ya leo…wasafiri walazimika kutembea kwa miguu

Baadhi ya wananchi wakazi wa Jijini Arusha wakionekana kutembea kwa miguu kuelekea maeneo ya mjini wanakofanyia shughuli za kila siku baada ya kukosa usafiri wa daladala  maarufu Jijini hapa kama Vifodi kulikosababishwa na mgomo wa wasafirishaji hao mapema leo asubuhi. Eneo lililoathirika na kadhia hiyo ni njia ya Kwamrombo, Mbauda, Majengo na njia ya Ngaramtoni hadi mjini.

Waendesha bodaboda walikuwa na muda mzuri wa mavuno kwa baadhi ya abiria waliolazimika kukodi pikipiki

Blog hii inaendelea kufuatilia kisa hasa cha mgomo huo na athari nyinginezo kama zipo. Picha na Shangwa Francis, Eliud Akyoo.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO