Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MBIO ZA NYIKA ZA MCHUJO ZAFANYIKA ARUSHA, KWA SAFARI YA KUIWAKILISHA JIJI LA ARUSHA MOROGORO

Kocha wa timu ya wanawake Arusha (kulia) akiwa tayari kumkabidhi namba mwanariadha anayemazila fainali ya mbio hizo.
Kwa mujibu wa viongozi wa riadha Mkoani Arusha huu ndio mchujo wa halali wa wanariadha wa timu ya Mkoa watakao uwakilisha mkoa wa Arusha katika mashindano ya riadha ya Nyika yatakayofanyika kitaifa Mkoani Morogoro hivi karibuni.
HAYA NDIO MATOKEO YA WANARIADHA WALIOCHAGULIWA...
KWA WANAUME: KILOMITA 8:
1. Peter Sulle - Amekimbia dakika -22:27:09 (JWTZ)
2. Nelson Priva -Dakika - 22:27:87 (Arusha Training Center)
3. Faustin Musa - Dakika - 22:49 (JWTZ)
4. Joseph Itambu - Dakika - 22:56 (JWTZ)
5. Uwezo James - Dakika - 22:59 (JWTZ)
6. Doto Ikangaa - Dakika - 23: 05 (JWTZ)
KWA WANAWAKE KILOMITA 8 ALIPATIKANA MMOJA TU.
1. Flora Yuda - Dakika - 29:53

Wilhem Gidabuday (mwanariadha mkongwe na mwana harakati wa michezo Tanzania) akiwaandikisha washindi mara baada ya kumaliza mbio zote. Kulia pia ni kocha wa timu ya JWTZ akiwa makini katika kutunza muda kwa wanariadha ili wamalize katika muda ulipangwa.
KWA UPANDE WA WANAUME - KILOMITA 4..
1. Agustino Sulle - dakika - 10:56 (Wining Spirit)
2. Mohamed Ali - dakika - 11:02 (JWTZ)
3. Paulo Paskali - dakika - 11:03 (Wining Spirit)
4. Mohamed Iddi -  (JWTZ)
5. Paskali Ramadhani (Wining Spirit)
6. Adam Husen (JWTZ)
KWA WANAWAKE - KILOMITA 4:
1. Angelina Tsere - dakika - 13:02 (Wining Spirit)
2. Fadhila Mtita - dakika - 13:17 (JWTZ)
3. Selina Amos - dakika - 13:32 (Wining Spirit)
4. Rosalia Fabian - (Wining Spirit)
5. Magdalena Crispian - (Wining Spirit)
6. Johari Ibrahim - (Wining Spirit).  

Kocha wa timu ya riadha ya wanawake Arusha  akimkabidhi namba mwanariadha wakati wa kumaliza fainali za mbio hizo

Baadhi ya washindi wa bio zote za majaribio ya kutafuta wanariadha watakao iwakilisha Arusha katika mashindano ya Nyika (kitaifa) yatakayofanyika hivi karibuni mkoani Mororogoro. Kutoka kulia ni mshindi wa kwanza hadi wa nne (wa nne ndiye msichana pekee.

Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Mkoa wa Arusha Bw. Jackson Busiru Jorwa ameahidi kuchukuwa medali zote kwa upande wa wanariadha wakubwa na wadogo.

Kocha wa "JWTZ" Bw. Antony Mwingereza akiwahusia wanaridha wa mkoa wa Arusha mara baada ya mashindano ya majaribio kumalizika vyema.
Kocha Antony pia ametoa wito kwa viongozi wa ngazi ya mkoa hapa Arusha kuwa na moyo wa kuhudhuria matukio kama haya, kwani itawapa wakati mzuri wa kuhakiki ripoti wanazokuwa wanaandikiwa na hivyo kuweza kufanikisha tasnia hii ya mchezo wa riadha hapa Arusha.

SIKILIZA MAHOJIANO YOTE WAKATI AKIZUNGUMZA NA ASILI YETU TANZANIA BLOG.

Kocha wa timu ya "Samsung" Samwel Tuppa akiwa na mkewe ambaye pia ni kocha wa timu ya wanawake mkoani Arusha - wote wakiwa katika mchakato wa kuchuja washiriki wa riadha jijini Arusha.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO