Rais Francois Bozize akizungumza na waandishi wa habari katika mji mkuu Bngui.
Waasi wa Jamhuri ya Afrika ya kati wamechukua udhibiti wa mji mkuu hivyo kumlazimu rais Francois Bozize kuikimbia Bangui.
Mashahidi wanaripoti kutokea mapigano makubwa katika mji huo Jumapili wakati waasi wanatafuta njia zao kuingia kwenye mji mkuu ili kuchukua udhibiti wa makazi ya rais.
Maafisa wa usalama hawakusema rasmi wapi alipokimbilia rais Bozize , lakini shirika la habari la kimataifa la Reuters limemnukuu mshauri wa rais akisema kuwa rais huyo alikatisha kuingia Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo mapema Jumapili.
Kundi la Seleka lilianza mashambulizi yake mwezi Desemba na kuchukua udhibiti wa eneo kubwa la nchi . Waasi hao baadae walifikia makubaliano na Serikali lakini wamemshutumu rais Bozize kwa kuvunja makubaliano hayo.
Bwana Bozize ameongoza jamhuri ya Afrika ya Kati tangu alipochukua madaraka kwa njia ya mapinduzi mwaka 2003.
Jamhuri ya Afrika ya kati ina historia mapinduzi na ghasia tangu ilipopata uhuru wake mwaka 1960
Chanzo: Voice of America/Africa
0 maoni:
Post a Comment