Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mbatia ajitoa Tume ya kuchunguza kushuka elimu

Mwenyekiti  wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia (pichani) amejitoa kwenye Tume ya serikali kuchunguza chanzo cha kushuka kwa kiwango cha kustisha cha matokeo ya kidato cha nne, iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Mbatia ambaye ametajwa kuwa mmoja wa wajumbe wa tume hiyo yenye wajumbe 15, alisema kamwe hatoweza  kufanya kazi yake kwa uhuru kwa sababu  ni Mbunge wa kuteuliwa, kamati hiyo imeundwa na serikali hivyo lazima kutakuwa na mgongano wa maslahi.

Hatua hiyo imekuja siku tatu baada ya chama hicho kumwandikia barua Rais Jakaya Kikwete, kikimuomba aunde tume ya kudumu ya elimu nchini.

Tume hiyo iliundwa kutokana na matokeo mabaya ya mtihani wa kidato cha nne,  watahiniwa 240,903 kati ya 480,036  waliofanya mtihani walipata alama sifuri, huku 23,520 sawa na asilimia 5.16 wakifaulu na wengine 103,327 sawa na asilimia 26.02 wakipata daraja la nne.


Januari 31, mwaka huu katika kikao cha bunge, Mbatia aliwasilisha hoja binafsi kuhusu udhaifu katika sekta ya elimu akielezea kwa kina, sera ya elimu iliyopitwa na wakati, kukosekana kwa mitalaa, kuwapo kwa mihtasari mibovu ya masomo na vitabu kuwa na viwango duni.

Hata hivyo, wabunge wa CCM wakishirikiana na Serikali walimaliza hoja hiyo   bila kutolewa majibu ya msingi.

Mbatia alisema jana kuwa hawezi kufanya kazi yake kwa ufanisi ndani ya tume hiyo, kwa sababu ndiye aliwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusu udhaifu sekta ya elimu,  hoja ambayo ilizimwa bila kutolewa majibu ya msingi.

“Kamati ya Waziri mkuu haina jipya la kufanya kwa sababu ipo Kamati iliyoundwa mwaka 2011 kuchunguza matokeo mabaya ya kidato cha nne,  imeeleza kila kitu na ripoti ipo ofisi ya waziri mkuu, sasa hii ya sasa inakwenda kuchunguza nini?” alihoji Mbatia.

Mwananchi

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO