Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

BREAKING NEWS: JENGO LA GHOROFA 16 LAANGUKA KATIKATI YA JIJI DAR ES SALAAM, YADAIWA WATU ZAIDI YA 60 WAMEFUKIWA NA KIFUSI

Jengo la Ghorofa 16 limeporomoka Jijini Dar mtaa wa Indira Ghand, kwa taarifa za awali inasemekana kuna watu ambao wamefunikwa na kifusi baada ya ghorofa hilo kuanguka, jitihada za kuokoa zinaendelea na mpaka sasa tayari wameokolewa majeruhi 16 na zimepatikana maiti mbili.

Kwa mujibu wa taarifa ya MilardAyo.Com ikinukuu maelezo ya shuhuda wa tukio, inasemekana jengo hilo limeanguka saa moja asubuhi ambapo kwa muda huo kulikua na watoto wa kihindi wanacheza mpira, kulikua na vibarua ambao wanataka kumwaga zege kuendelea na ujenzi na ndio walikua wanabadilisha nguo kuanza kazi.

Ni posta mtaa wa Indira Gandhi pembeni ya msikiti mkubwa wa Itnasheri, lilikua ni gorofa la floor 12 ambapo mpaka sasa hakuna hesabu kamili ya vifo lakini shuhuda anasema kwa muda mfupi baada ya kuanguka alishuhusia maiti nne.

Sehemu ya chini zinaonekana bado nzima hazijadondoka ila kifusi cha kutoka juu ndio kimefunika lakini kuna watu ndani yake wako hai na inaripotiwa wanapata hewa vizuri na wamekua wakiwapigia ndugu zao na kuwaita waje kwenye eneo la tukio.

Endelea kuwa nasi kwa taarifa zaidi

Mtoto Maisamali Karim (6) ambaye ameokolewa kutoka katika madrasa ya Msikiti wa Khoja Shia Ithna Asheri Jamaat iliyoangukiwa na jengo hilo katika mtaa wa Indira Gandhi. (Picha zote na Habari Mseto Blog)

Changamoto ya uokoaji ni ngumu, lakini vikosi mbalimbali vinaendelea na zoezi hilo, ili kunusuru maisha ya waliofukiwa na kifusi.

Hizi nia aina ya nondo ambazo kimsingi sio imara kuweza kuhimili ujenzi wa ghorofa ndefu kama hili, kuna haja mamlaka husika likatupia macho kampuni za ujenzi ili kuokoa maisha ya wajenzi na watumiaji wa majengo hayo.

Askari wakiimarisha ulinzi wakati zoezi la uokoaji likiendelea.

Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea, huku nondo nyembamba zikionekana na kuacha maswali miongoni mwa mashuhuda wa tukio hilo.

Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea.

Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea.

Waokoaji.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam (CP), Suleima Kova kuhusu jengo la ghorofa 16 lililoanguka majira ya saa mbili asubuhi katika makutano ya mtaa wa Indira Ghandi na Barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi. Katika ajali hiyo watu wawili wamekufa papo hapo.

Waokoaji wakiwa kazini.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum (CP), Suleima Kova.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum (CP), Suleima Kova akiwa katika eneo la tukio. Kulia ni Mbunge wa Kuteuliwa na Rais (NCCR-Mageuzi) Mh James Mbatia.

PICHA ZOTE NA FRANCIS DANDE HABARI MSETO BLOG

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 maoni:

The P said...

Ingawa kila kitu hupangwa na M/Mungu ila M/Mungu nae hutuambia hamtopata matatizo ila chanzo ni nyinyi wenyewe, na leo hii ndo haya yanatokea kila kukicha . Mara Nungwi kisa ni Overloading, Mara Mabomu kisa Uchunguzi , Mara Ghorofa kisa rushwa, Mara Umeme kisa Nishati,Mara Mahospitalini kisa migomo, Mara Kufeli kwa wanafunzi kisa Tasisi, Mara Mauwaji kisa ulinzi mdogo, haya sasa hivi utasikia Njaa kisa kupanda bei kwa vyakula.Eeeeeeee...................Tumechoka, mbona hivi? au ndo miaka 50 ya uhuru????

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO