Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Taarifa Kwa Umma: Kampeni ya ushirikishwaji wananchi katika uzazi salama,"Mama Ye!" yazindua tovuti

KILA UTAFITI UNAANZA NA SWALI LA KAWAIDA KABISA

Na hivyo ndivyo tunavyotakiwa kuanza na sisi.

Ni nini kinachoua japo mwanamke mmoja katika takriban kila saa?

A: UKIMWI

B: SARATANI

HAKUNA JIBU HATA MOJA HAPO JUU

C: JIBU NI UJAUZITO NA KUJIFUNGUA

Wanawake 23 hufariki kila siku nchini Tanzania kwa sababu zinazohusiana na ujauzito na kujifungua. Jambo gumu kabisa kulikubali hapa ni kuwa kuleta uhai wa kizazi kijacho ndio chanzo kikuu cha vifo kwa wanawake wa Tanzania.

Na mara nyingi vifo hivi vingeweza kabisa kuzuilika: kutokwa na damu nyingi, uambukizo, huduma duni za tiba na elimu duni bado ndio kiini hasa cha janga hili. Wanawake fukara zaidi duniani ndio walio hatarini zaidi kufa. Ila wanawake hao sio wahanga pekee. Watoto wanaozaliwa nao wako hatarini kufa kwa kuwakosa mama zao.

MENGI zaidi yanahitajika kufanyika kuwaokoa hao mama na watoto wao. MENGI hasa.

Leo (22 Machi), Mama Ye!, kampeni ya kushirikisha umma kuchukua hatua za kuokoa akina mama na vichanga wa Tanzania inazindua tovuti yake. Hii ni sehemu ya kwanza ya kampeni inayoendeshwa barani Afrika kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano ya simu kushirikisha watanzania wa kawaida katika vita hii muhimu—vita ya kupambana na vifo vya akina mama na watoto wachanga.

Nchini Tanzania, ambako kuna sera madhubuti na mpango kabambe ya kushughulikia afya ya wajawazito, Shirika la Afya Duniani linakadiria kuna wanawake 8,500 wanaofariki kila mwaka wakati wakileta uhai mwingine hapa duniani. Yaani ukweli huu unaoumiza ni kuwa

kitendo cha kujifungua huwa ni jambo la kutia shaka miongoni mwa wajawazito wengi na familia zao hapa nchini.

Mama Ye! (www.mamaye.or.tz) ni kampeni ya kuelimisha na kuhamasisha jamii kuchukua hatua kwa umoja wao na kila mmoja binafsi, kwa ajili ya kuwasaidia wajawazito miongoni mwao. Itajaribu kuiondosha dhana kwamba jukumu la uhai wa wajawazito liko mikononi mwa ‘serikali’ ‘wizara’, ‘wataalamu’ ‘Umoja wa Mataifa’ au wafadhili pekee yao. Kwa Mama Ye! ushiriki wa kila Mtanzania ni kiini cha mafanikio.

Teknolojia inaweza kusaidia kuhamasisha jamii kuchukua hatua za moja kwa moja katika kulikabili janga la vifo vya mama na watoto wachanga. Mama Ye! inazingatia uwepo wa simu za mkononi bilioni moja, watumiaji mtandao 167,335,676 na waliojisajili na Facebook wapatao 51,612,460 watakaokuwepo barani Afrika ifikapo mwaka 2016. Nchini Tanzania matumizi ya simu za mkononi yameshafikia asilimia 52% ya wakazi wote na idadi hii inaendelea kuongezeka.

Mama Ye! imezinduliwa na mradi wa Evidence for Action, ambao unafadhiliwa na Kitengo cha Maendeleo ya Kimataifa cha Serikali ya Uingereza. Mkurugenzi wake nchini Tanzania Craig Ferla amesema:

“Wote tuna uwezo na nguvu ya kuokoa maisha kama ambavyo wameonyesha madereva taxi wanaowawahisha wajawazito hospitali kujifungua; au kama ambavyo wameonyesha wanaochangia damu kwa hiari kuokoa maisha ya kina mama na watoto.

Kujifungua si ugonjwa. Tumetambua kwa miongo kadhaa sasa kuwa ni nini kinatakiwa ili kuhakikisha mama na watoto wachanga wanaishi. Lakini kama tunataka waishi basi jamii ya watanzania inatakiwa kuchukua hatua na kujihusisha tena kwa kujituma.

Mama Ye! itatoa ushahidi, taarifa na nyenzo muhimu kwa ajili ya kuleta mabadiliko.

Na teknolojia mpya itawasaidia watanzania kuchukua hatua kwa namna ambayo miaka ya nyuma ilikuwa ni kama ndoto.”

Baadhi ya wananchi wa Arusha waliojitolea damu siku ya uzinduzi wa kampeni ya Mama Ye! Jijini Arusha mapema mwwaka huu

"Mstahiki Meya Jerry Silaa akiwa amepakata mtoto wa Bi. Halima Abubakary mkazi wa Kata ya Gongo la Mboto katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala aliyejifungua salama usiku wa kuamkia Machi 19, 2013 kwenye Zahanati iliyojengwa na Mstahiki Meya ikiwa ni kutekeleza ahadi zake kwa wapiga kura wake."--Habari hii kwa hisani ya Dewji Blo

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO