Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

SAFARI YA MWISHO YA MJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM BENSON MOLLEL

Clip 4

Viongozi wa Dini (Wachungaji) wakifanya maombi ya mwisho kabla ya kuuhifadhi mwili wa aliyekuwa Mjumbe  wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (Uvccm), ngazi ya taifa  kupitia mkoa wa Arusha, Benson Mollel (26) aliyeaga dunia hivi karibu

Clip 5

Baadhi ya Viongozi walio hudhuria mazishi ya Mjumbe  wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), ngazi ya taifa  kupitia mkoa wa Arusha, Benson Mollel (26) aliyeaga dunia hivi karibu katika hoteli ya Lush Garden Bussines Hotel iliyopo barabara ya vijana mkabala na  Jacaranda  mtaa wa Haile Selassie katikati ya jiji la Arusha

Clip 10

Clip 11

Clip 12

Clip 16

Clip 22

Mama Mzazi wa Marehemu Benson Mollel akiwa analia kwa uchungu baada ya kuweka shada la maua juu ya kaburi la mwanaye

Clip 23

Mama Mzazi wa Marehemu Benson Mollel akiwa anashikiliwa na wasaidizi katika mazishi

Clip 25

Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas akiwa anatoa heshima za mwisho mara baada ya kuweka shada la maua

Clip 26

Mstahiki Meya wa jiji la Arusha Gaudence Lyimo akiweka shada la maua kwenye kaburi.

Clip 31

Clip 34

Naibu waziri wa nishati na madini Steven Masele katikati aliye valia nguo ya kijani na miwani akishuudia mazishi ya Benson Mollel

Clip 35

Clip 37

Mama na Baba Mzazi wa Marehemu Benson Mollel nao wakiweka shada la maua kwenye Kaburi la mwanaye.

Clip 38

Mfanya biashara wa madini maarufu jijini Arusha Bw. Mathias Manga akiwa na Mkewe wakiweka shada la maua kwenye kaburi la Marehemu Benson Mollel

Clip 40

Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli Mh.Edward Lowassa akiwa amebeba shada la mau kabla ya kuweka kaburini.

Clip 44

Naibu waziri wa ardhi nyumba na makazi Godluck Ole medeye mwenye miwani akiwa amebeba shada la mau kabla ya kuliweka kwenye kaburi

Clip 45

Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo akipeleka shada la maua kwenye kaburi.
Clip 49
Mstahiki Meya wa jiji la Arusha Gaudence Lyimo akiweka shada la maua kwenye kaburi.
Maelfu ya wananchi wakiwemo viongozi mbalimbali wa kitaifa, viongozi wa dini, vyama vya siasa walijitokeza kumzika aliyekuwa Mjumbe  wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(Uvccm),ngazi ya taifa  kupitia mkoa wa Arusha ,Benson Mollel (26)aliyeaga dunia hivi karibu katika hoteli ya Lush Garden Bussinnes Hotel iliyopo barabara ya vijana mkabala na  Jacaranda  mtaa wa Haile Selassie katikati ya jiji la Arusha.
Viongozi walioudhuria msiba huo jana nyumbani kwa marehemu katika kata ya Lemara jijini Arusha ni pamoja na Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli Mh.Edward Lowassa, Naibu waziri wa ardhi nyumba na makazi Godluck Ole medeye, Naibu waziri wa nishati na madini Steven Masele, Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo, Mstahiki Meya wa jiji la Arusha Gaudence Lyimo pamoja na viongozi mbalimbali wa UVCCM Taifa na Mkoa.
Msiba huo ulikuwa wa aina yake kutokana msururu wa magari pamoja  na umati mkubwa  wa watu kufika hali iliyopelekea wananchi  wengine kushindwa hata kuaga mwili wa marehem kutokana na ufinyu wa eneo hilo
Katika salamu za rambirambi Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha Robinson Meitenyiku alisema kuwa marehemu ameacha pengo kubwa sana kwana UVCCM na hata kwa wananchi huku akiwataka vijana kumrudia Mungu kutokana na vijana wengi kufa kwa umri mdogo hali ambayo inapelekea nguvu kazi ya taifa kupungua.
“Benson alikuwa mjumbe wa baraza mkoa,kamati ya utekelezaji mkoa na mjumbe wa baraza Taifa tunajua alikuwa na malengo gani na ndiyo tutaenda kuyafanya kwasababu alikuwa ni kiongozi mpenda maendeleo katika jamii”Alisema Meitenyiku
Hata hivyo aliweka wazi kwa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete kuwa toka aingie madarakani pamoja na marehemu hakujawahi kuwepo na makundi katika UVCCM mkoa wa Arusha
“Tunamshukuru Rais kwa salamu zake ila ajue kuwa toka Robinson na Benson waingie madarakani hatujawahi kuwa na makundi ya aina yeyote ile hivyo ushindi uko pale pale”alibainisha  Meitenyiku
Kwa upande wake Naibu waziri wa ardhi nyumba na makazi Goodluck ole Medeye aliwataka vijina kutokukata tama pamoja na kuzingatia elimu inayotolewa na viongozi wa dini,serikali ili kuepuka uvunjifu wa amani hapa nchini.
“Marehemu alikuwa ni mfano mzuri wa kuigwa kutokana na alipenda amani…..Nilipopata taarifa kuwa Benson amefariki nilijiwa na picha ya mgomba mchanga uliyochipua ulipokaribia kuchanua ukakatwa ghafla …..matunda ambayo tulitarajia kuyapata katika mgomba huo hatujayapata “alisema

Aidha aliwakumbusha vijana mshikamano pamoja na upendo miongoni mwao huku akiwataka watumie ujuzi walionao katika kuliendeleza Taifa na kuondoa umaskini.

PICHA: JAMII BLOG, ARUSHA

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO