Kulia wa pili ni diwani wa kata ya Unga ltd Mh.Issa Saidi akisalimiana na Afisa masoko na matukio wa kampuni ya Megatrade Jailos Joseph kama ishara ya shukrani baada ya kampuni hiyo kukabidhi msaada wa sufuria mbili kwa shule ya Msingi Ungaltd zenye thamani ya zaidi ya shilingi Mil.2 kulia wa kwanza aliyevalia kitenge ni Ester Rodrick – Afisa Elimu Kata ya unga ltd,kushoto ni Joachim Kisarika – Afisa Mtendaji kata ya unga ltd na Kakwaya Ruji – Afisa wa shughuli maalum za Megatrade Inv. ltd
Hapa picha ikionyesha wafanyakazi wa Megatrade pamoja na uongozi wa kata na shule wakiwa katika picha ya pamoja kushoto ni Happiness Kimaro ambaye ni secretari wa kampuni
Msaada huo umekuja baada ya uongozi wa kata pamoja shule kuandika barua kwa kampuni hiyo kuomba msaada wa sufuria mbili za ujazo wa lita 100 na lita 200 kwaajili ya kuwapikia chakula wanafunzi wakiwa shuleni, kutokana na wanafunzi kushinda njaa kwa muda mrefu na kushindwa kumudu masomo yao vizuri hali inayopelekea wakati mwingine kuanguka na kupoteza fahamu na wengine kutoroka shule kutokana na njaa
Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya kampuni Afisa masoko na matukio wa kampuni ya megatrade Bw Jailos Joseph alisema kuwa kampuni imeguswa na hali hiyo ya wanafunzi kukosa chakula shuleni na kusababisha baadhi yao kutoroka mchana au kushindwa kufwatilia vizuri masomo yao kutokana na njaa huku akiweka wazi kuwa ukiwa na njaa huwezi kutuliza akili darasani na hivyo kuchangia kushuka kwa ufaulu wa watoto katika mitihani yao.
Hata hivyo alisema kuwa kampuni iliitikia wito huo ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa kurudisha kwa jamii kile kidogo kinachopata kutokana na kuuza bidhaa zake za K-Vant Gin na Kiroba Original ikatoa sufuria hizo 2 za ujazo wa lita 200 kila moja zenye thamani ya zaidi ya 1,200,000 ili kunusuru hali ya elimu katika kata hiyo ya unga ltd na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wa Kata, Diwani alisema wanafanya utaratibu wa mkutano wa kamati ya shule , kata, wazazi na wanafunzi wote kuwaonyesha na kuwakabidhi msaada huu ambapo watawaita na kututambulisha kwao, kuwa wao ndo waliotoa msaada huo huku akitoa neno la shukrani kwa kampuni ya Megatrade kwa niaba ya kata na shule
PICHA NA STORI: PAMELA MOLLEL
0 maoni:
Post a Comment