Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Lowassa, Mengi, kufanyiziwa kama Kibanda, Lwakatare • Afisa Ikulu ahusishwa na mkakati huo, afya ya Lwakatare mbaya

WAKATI sakata la Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare anayetuhumiwa kupanga mikakati ya uhalifu na kurekodiwa kwa video likizidi kuibua maswali, vigogo wengine wanadaiwa kuandaliwa mpango wa kurekodiwa kwenye video ili kuwachafua na kuwanyamazisha, Tanzania Daima Jumapili limebaini.

Vigogo hao ni pamoja na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi, Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe.

Taarifa za mkakati huo zilisambazwa jana kwenye mtandao maarufu wa Jamii Forum, huku ukihusisha mawasilino ya ofisa mmoja wa Ikulu ya Rais Kikwete akieleza kufurahishwa kwake na kuwapongeza waliofanikisha mpango wa kuandaa video ya Lwakatare ambaye kwa sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi.

Kunaswa kwa mawasiliano hayo kunaibua hisia kwamba huenda picha za video za Lwakatare zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ndani na nje ya nchi zikionesha mipango ya kufanya uhalifu ni ya kughushi.

Kwa mujibu wa habari hizo kuna mkakati mkubwa unaosukwa na baadhi ya watumishi wasio waaminifu wa vyombo vya dola, kutengeneza video nyingi kwa watu mbalimbali kuwahusisha na ufadhili wa vitendo vya uharamia na kuwateka na kuwadhuru kama alivyofanyiwa hivi karibuni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari, Absalom Kibanda.

“Mtu wangu wa karibu ameniambia kuwa wana mpango wa kumtengenezea video kama hiyo, Mengi, Lowassa na Freeman Mbowe ili kuwanyamazisha,” ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo.

Mbali ya kuandaliwa video chafu kama Lwakatare, imedaiwa kuwa Lowassa, Mengi na Mbowe wanatengenezewa fitna kuionesha jamii kwamba wanafadhili genge la kijasusi linalosababisha mauji ya raia nchini.

Tangu kuibuliwa kwa kashfa ya video ya Lwakatare, baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamekuwa wakipinga propaganda za chini kwa chini kuihusisha CHADEMA na matukio ya kijasusi ya kuuawa kwa baadhi ya raia na waandishi wa habari, likiwemo tukio la hivi karibuni la kuvamiwa na kupigwa kwa Kibanda ambaye kwa sasa anatibiwa nchini Afrika Kusini.

Duru za uchunguzi zinaeleza kuwa mchezo mzima wa mkanda wa video ya Lwakatare na kuvamiwa na kupigwa kwa Kibanda, unadaiwa kuchezwa na watumishi wachache wasio waaminifu ndani ya vyombo vya dola.

Uthibitisho wa madai hayo unatokana na mawasiliano ya ofisa mmoja wa Ikulu ambaye jana mawasilino yake ya siri na watu mbalimbali yalinaswa akiwapongeza vijana walioandaa video ya Lwakatare na kutaka viongozi wa CHADEMA wakamatwe na kwamba hiyo ni kete kubwa kwa CCM.

Hata hivyo kasoro moja ya mawasiliano hayo ni kwamba mtoa habari hakuweka kopi halisi wa hayo mawasiliano badala yake aliweka faili ambalo liko kwenye mfumo wa PDF.

Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu alipotafutwa kwa simu kuzungumzia taarifa hiyo na kuhusishwa kwa ofisa mmoja wa Ikulu, hakuweza kupatikana.

Wakati huohuo, hali ya afya ya Lwakatare ni mbaya.

Imeelezwa kuwa hali ya kiongozi huyo imezorota kutokana na kiwango cha sukari kupanda.

Taarifa zilizothibitishwa na wakili wake na watu wake wa karibu, zinasema kuwa hali yake ni mbaya na Jeshi la Polisi lilikuwa likifanya utaratibu wa kumkimbiza hospitalini ili aweze kupatiwa matibabu.

“Hali ya Lwakatare ni mbaya, sukari imepanda sana, kwa hali yake hii ya ugonjwa tunatafuta uwezekano wa Jeshi la Polisi kumpeleka hospitalini, ingawa bado hawajakubali au kuonyesha kuwa wanampeleka hospitalini,” alisema wakili wake, Nyaronyo Kicheere.

Jana gazeti hili liliripoti taarifa ya Kicheere akisema pamoja na polisi kumshikilia Lwakatare, walikuwa wamemweka katika mahabusu isiyokidhi hali ya afya ya kiongozi huyo, ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari.

Alisema: “Hali ya Lwakatare ni mbaya, anaumwa kisukari, anahitaji chakula kila baada ya saa nne, na kupata huduma ya haja ndogo mara kwa mara, lakini amewekwa katika chumba ambacho hakina huduma ya choo ingawa vinapatikana pale polisi.

“Ni kinyume cha sheria kumweka mtu polisi saa zote hizo, na wanafanya vile utadhani huyu wameshamtia hatiani. Hatuwezi kuhamishia familia yake pale ili wampatie chakula kila mara.”

Aliongeza kuwa juzi alipotolewa kutoka katika chumba alipohifadhiwa alikuwa na hali mbaya kiasi cha kushindwa kuongea au kusimama kwa kuwa alikuwa hajala kwa muda mrefu kulingana na hali ya ugonjwa wake.

“Mtu wa aina hii sio wa kuwekwa mahabusu muda mrefu, kwanza Lwakatare sio mtu wa kutoroka, ukiachilia mbali suala la kisheria linalowalazimisha polisi kumpeleka mahakamani ndani ya saa 24,” alisema.

Gazeti hili lilimtafuta Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu, Suleiman Kova kuhusu suala hilo na akasema: “Sisi hatuna haja ya kuletewa maombi na upande wowote, mahabusu yeyote anayeumwa anapelekwa hospitalini, sisi tunakagua chumba cha mahabusu kila baada ya nusu saa, tunakagua afya tukikuta kuna mgonjwa basi anapelekwa hopitali, ila kwa suala hasa la Lwakatare wasiliana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala.”

Kamanda wa Ilala, Marietha Minangi, alipoulizwa alisema: “Tulipata taarifa tangu jana tukaenda kumwambia tumpeleke hospitali, lakini akasema anajisikia vizuri. Suala hilo sio lazima mpaka vyombo vya habari vitusaidie kuuliza, sisi tunajua wajibu wetu.”

Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi linamshikilia Ludovick Joseph, mfanyakazi wa blogu ya Mjengwa, akihuhushwa na tuhuma za kuvamiwa na kupigwa kwa Kibanda.

Hata hivyo bado kuna utata wa sababu hasa iliyomfanya Ludovick kukamatwa na polisi.

Habari za kipolisi zinasema kuwa mtuhumiwa huyo amekamatwa akihusishwa na tukio la kupigwa Kibanda wakati taarifa zingine zikisema ameunganishwa na Lwakatare akidaiwa kuandaa mipango ya uhalifu

Chanzo: Tanzania Daima Jumapili, Machi 17, 2013

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO