Waratibu wa bonanza la vijana Jijini Arusha linalotarajiwa kufanyika Machi 30, 2013. Sayuni Wiliam, Immanuel na Mathias Paul wakizungumza na blog hii jana.
****************
Katika kuelekea sikukuu ya Pasaka, Vijana wa Jijini Arusha kupitia umoja wao ‘Vijana Kwa Pamoja Tunaweza’ kwa kifupi VIPATU wameandaa siku maalumu kujumuika pamoja kwa michezo mbali mbali sambamba na kupata wasaa wa kuwa karibu na viongozi wa kijamii Jijini hapa katika viwanja vya wazi Soweto.kuanzia saa 3 asubuhi.
Katika siku hiyo (Macho 30, 2013) inaelezwa kuwa kutakuwepo na michezo ya aina mbalimbali ikishirikisha makundi mbali mbali ya kijamii na kwamba kila mwananchi atakayehudhuria siku hiyo ataruhusiwa kushiriki mchezo atakaoupenda
Akizungumza na Blog Hii, Mratibu wa Bonanza hilo Doris Kessy amestaja baadhi ya michezo inayotazamiwa kushindaniwa siku hiyo ni pamoja na mpira wa miguu, mpira wa pete, kurusha vitu vizito, kukimbiza kuku na kukimbia na magunia.
Michezo mingine ni mpira wa kikapu, mbio za miguu mitatu, kukimbia na fimbo, sarakasi na kuruka kamba.
Doris anasema watu wote hususani vijana wa Arusha wanaalikwa kuhudhuria na kushiriki bonanza hilo la bure na kwamba majina ya washiriki wa michezo mbalimbali yataorodheshwa asubuhi viwanjani hapo siku ya bonanza.
Mratibu huyo aliwataja baadhi ya wadhamini ambao wamethibitisha kusaidia Bonanza hilo ni pamoja na Pepsi, Maezeki, Angaza, pamoja na Yes Tanzania.
Blog hii inafuatilia zaidi kuhusu Bonanza hili na kukujuza zaidi!
0 maoni:
Post a Comment