Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MJUMBE WA BARAZA KUU LA UMOJA WA VIJANA UVCCM NGAZI YA TAIFA MKOA WA ARUSHA ALIVYOKUTWA AMEKUFA KATIKA HOTEL YA LUSH GARDEN BUSINESS JIJINI ARUSHA

benson mollel

Aliyekuwa mjumbe wa baraza kuu la Uvccm mkoani Arusha,Benson Mollel aliyevalia shati la kung’aa tofauti na wenzake akitoa msaada kwa mtoto aitwaye frank wakati jumuiya hiyo ilipofanya ziara ya kutembelea wagonjwa katika hospitali ya mkoa ya Mt meru hivi karibuni enzi ya uhai wake,anayefuatia ni mwneyekiti wa uvccm mkoani hapa,Robinson Meitenyiku

***************

MJUMBE  wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(Uvccm),ngazi ya taifa  kupitia mkoa wa Arusha ,Benson Mollel(26) amekutwa amefariki dunia ndani ya hoteli ya Lush Garden Bussinnes Hotel iliyopo barabara ya vijana mkabala na  Jacaranda  mtaa wa Haile Selassie katikati ya jiji la Arusha.

Tukio hilo lililogusa hisia za wengi  lilitokea  ghafla leo (jana) 3/3/2013  majira ya saa 6:oo mchana  tayari limezua hali ya hofu na mashaka kwa wakazi wa jiji la Arusha na viunga vyake ambapo tayari limehusishwa na hisia mbalimbali ikiwemo kulishwa sumu kali.

Kabla ya kukutwa na umauti alikuwa ni mwanasiasa  mchanga ambaye pia alikuwa ni mfanyabiashara wa madini mkoani hapa ambapo kifo chake kimehusishwa na masuala ya kisiasa na kibiashara

Marehemu Mollel,aliutwaa ujumbe wa baraza kuu la Uvccm mkoani Arusha mwaka huu huku akimrithi mkuu wa wilaya ya Korogwe kwa sasa,Mrisho Gambo katika uchaguzi uliokuwa na mshike mshike huku akitajwa kuwa kambi ya waziri mkuu mstaafualiyejiuzulu,Edward Lowasa.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari ndani ya hoteli hiyo vimedai ya kwamba marehemu aliwasili mnamo machi 2 mwaka huu majira ya usiku hotelini hapo akiongozana na mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Nancy ambapo walichukua chumba nambari 214.

Mmmoja wa walinzi hotelini hapo aliyejimbulika kwa jina la Obeid Mollel kutoka kampuni ya ulinzi ya Victoria Support Services ambayo inaimarisha ulinzi hotelini hapo alisema kuwa marehemu aliingia na mwanamke huyo na kisha kuondoka ghafla kabla ya kurejea tena wakiwa wote usiku.

Hatahivyo,alisema kuwa wakati wakiwa hotelini hapo marehemu aliomba kuegesha gari lake jipya ambalo bado halijapata usajili lenye nambari 4093 gx 110 aina ya mark ii grande ambapo alikubaliwa na kisha kurejea chumbani na mwanamke huyo ambaye anatajwa kuondoka leo  asubuhi 3/3/2013

Hatahivyo,majira ya asubuhi mmoja wa wahudumu hotelini hapo(jina lake limehifadhiwa) alisema kuwa mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Maryam aliwasili hotelini hapo majira ya saa 5;00 na kuomba kupelekwa moja kwa moja chumba alichokuwepo marehemu. 

Mhudumu huyo kwa sauti ya upole alisema kuwa wakati mwanamke huyo akiomba kupelekwa chumbani hapo marehemu naye alipiga simu mapokezi na kuomba mwanamke huyo apelekwe chumbani kwake ambapo walitekeleza jukumu hilo.

Akiendelea kusimulia tukio hilo mhudumu huyo alisema kuwa walimwona mwanamke huyo akitoka ghafla nje ya hoteli hiyo majira ya saa 6;00 mchana bila kumtambua sura yake ambapo hawakufuatilia chochote kwa kujua kwamba hakuwa na nia mbaya.

 

“Sisi baada ya kumwelekeza Yule dada chumba alichofia marehemu hatukufuatilia hadi pale mlinzi alipomwona akitoka tena nje ya geti wala hakukaa muda mrefu”alisema mhudumu huyo

Hatahivyo,wakati hayo yakiendelea mhudumu huyo aliamua kupiga simu ya chumba alichofia marehemu ili kujua  endapo ataendelea kukodisha chumba hicho ama la lakini katika hali isiyo ya kwaida simu ya chumba hicho ilikuwa haipokelewi.

Wakati hayo yakiendelea alisimulia kwamba mmoja wa wahudumu ambaye alikuwa akifahamiana na marehemu kwa muda mrefu aliamua kumpigia kupitia simu yake ya mkononi lakini nayo haikupokelewa vilevile.

Baada ya hatua hiyo mhudumu huyo aliamua kupanda ngazi kwenda chumbani kwa marehemu lakini katika hali isiyo ya kawaida alikuta mlango ukiwa wazi na mara alipomwamsha marehemu hakuweza kuamka na ndipo alipotoa taarifa kwa uongozi wa hoteli na kisha kuviarifu vyombo vya usalama.

Hatahivyo,mhudumu huyo alipohiojiwa na jamiiblog.co.tz alisema kwamba anahisi nini chanzo cha kifo cha marehemu huyo alisema kuwa huenda mwanamke aliyekuwa naye (Maryam) huenda alitekeleza mauaji hayo kwa ustadi mkubwa bila wao kufahamu.

“Unajua vyumba vyote vya huko juu ghorofani ukifunga mlango tu huku chini sisi mapokezi tunasikia sasa cha ajabu mlango tumeukuta wazi na nahisi alitekeleza haya mauaji akaona asifunge mlango kwa kuwa tutasikia”alisema mhudumu huyo kwa upole

Jeshi la polisi liliwasili hotelini hapo majira ya saa  8;00 mchana na kuupakia mwili wa marehemu kupitia gari lenye nambari za usajili 1477 na kisha kuufikisha katika chumba cha kuhifadhia maiti ndani ya hospitali ya mkoa ya Mt,Meru

Akizungumza katika eneo la tukio mkuu wa jeshi la polisi wilayani Arusha,OCD Gilles Muruta alisema kwamba jeshi la polisi bado linachunguza undani wa tukio hilo kwa kuwa limejitokeza ghafla na hapo baadaye litatoa taarifa mwa vyombo vya habari.

Hatahivyo,katibu mwenezi wa CCM mkoani Arusha,Isaack Kadogoo alisema kuwa wao wamepokea tukio hilo kwa mshtuko mkubwa kwa kuwa bado wamepigwa na mashangao kwa jinsi namna lilivyotokea.

Baadhi ya wanasiasa wa vyama mbalimbali vya siasa pamoja na wafanyabiashara wa madini mkoani Arusha waliwasili eneo la tukio nje ya hoteli hiyo ambapo wengine walishindwa kujizuia na kujikuta wakiangua kilio nje ya hoteli hiyo.

Baadhi yao,James ole Milya kada wa Chadema pamoja na Mathias Manga diwani wa CCM kata ya Mlangarini wanaotajwa kuwa karibu na marehemu wakati wa uhai wake walionyeshwa kushtushwa na tukio hilo ambapo walikutwa wakitafakari nje ya hoteli hiyo.

Uongozi wa hoteli hiyo ulipotafutwa ili kutoa ufafanuzi juu ya tukio hilo uligoma kuzungumzia kwa madai kwamba limefikishwa mbele ya vyombo vya usalama.

DSCF8027

Muonekano wa nje ya hotel ya Lush Garden Business Hotel

DSCF8016

Chumba alichofia marehemu namba 214

DSCF8020

DSCF8026

jamiiblog inawapa pole nyingi familia ya  marehemu pamoja na ndugu na jamaa kwa msiba huo mkubwa,,,,Ndugu mdau wa blog hii tutaendelea kukuletea habari zaid juu ya msiba huo

CHANZO: JAMII BLOG (PAMELA MOLLEL)

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO