Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

KINANA NA TIMU YAKE WAENDELEA NA ZIARA YAKE NANCHONG, NCHINI CHINA

1AKatibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, akiwasalimia wazee katika kijiji cha mradi wa wakulima wa kupunguza umasikini cha Nanchong, jimbo la Sichuan, China, alipotembelea kijiji hicho, Machi 16, 2013. Anayemsalimia ni Ning Xiu (78). Kinana yupo nchini China na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya nyanja mbalimbali za kimaendeleo, kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha nchi hiyo cha CPC.
 1BKATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipata maelezo kuhusu shughuli za  kilimo alipotembelea mji wa Dantong, Nanchong kwenye miradi ya kilimo kwa ajili ya kupambana na umasikini, Machi 16, 2013. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai. Kinana yupo nchini China na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya nyanja mbalimbali za kimaendeleo, kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha nchi hiyo cha CPC.
 3Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha China, jimbo la Sichuan, Zhang Ning, wakitazama kazi za watoto, katika shule ya awali katika kijiji cha Dantong, wilaya ya Nanchong, Kinana na ujumbe wake walipotembelea miradi ya kilimo kwa ajili ya kupunguza umasikini, katika kijiji hicho, Machi 16, 2013.Kinana yupo nchini China na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya nyanja mbalimbali za kimaendeleo, kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha nchi hiyo cha CPC.
 4Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Amina Makilagi, akitazama vifaa vya michezo ya watoto katika shule ya  awali ya Kijiji cha Dantong, jimbo la Sichuan, Msafara wa Kinana ambao Amina yumo, ulipotembelea kijiji hicho kuona shughuli za mradi wa kilimo wa kupunguza umasikini, Machi 16, 2013. Kinana yupo China na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya nyanja mbalimbali za kimaendeleo, kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha nchi hiyo cha CPC. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk. Asha-Rose Migiro, na Watatu kushoto ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM , Khadija Aboud.
 5Katibu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitazama moja ya mashamba makubwa ya wakulima walipo kwenye mradi wa kupunguza umasikini, katika Kijiji cha Dantong, Jimbo la Sichuan, China, Machi 16, 2013. Kinana yupo nchini China na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya nyanja mbalimbali za kimaendeleo, kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha nchi hiyo cha CPC.
 6Wakulima  Kijiji kinachoendesha mradi wa kupambana na umasikini wa kilimo cha Nanchong, jimbo la Sichuan, wakiwa kazini Machi 16, 2013.
 7.KILICHO CHA AINA NTAKIPELEKA MKONI KWANGU”, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu akisema wakati akiwa kando ya shamba la kisasa la njegere, katika kijiji cha Nanchong, Jimbo la Sichuan, China, Machi 16, 2013. Jesca yupo katika msafara wa viongozi 14 wa CCM unaongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana nchini China.
 8Shamba la kabichi katika kijiji cha Nanchong, jimbo la Sichaun, China, Shamba hilo lipo katika mradi wa kupunguza umasikini katika kijiji hicho unaofanywa na serikali ya Jimbo la Siachuani ya Chama Cha Kikomunisti cha China. (Picha zote na Bashir Nkoromo)
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO