MKUU WA WILAYA YA MBOZI MKOANI MBEYA DR. MICHAEL KADEGE AKIONGEA NA WANAKIJIJI CHA MLOWO MBOZI
Mkuu wa wilaya ya mbozi mkoani mbeya dr. Michael kadege amejikuta kwenye hali ngumu baada ya wananchi wa kijiji cha mlowo kumzomea na kuvuruga mkutano wa kijiji ambao ulikuwa na madhumuni ya kutatua mgogoro uliodumu kwa mwaka mmoja baina ya kijiji hicho na halmashauri ya wilaya kuhusiana na makusanyo ya ushuru kwa wafanya biashara.
Aidha wananchi hao wamepinga kitendo cha mkuu wa wilaya kumsimamisha mwenyekiti wa kijiji bwana daud katule kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za kijiji , kutosoma mapato na matumizi pia kuchapisha vitabu vya kukusanya pesa na kutowasilisha fedha katika ofisi ya almashauri.
Kadege amesema sababu hizo ndizo zilimpelekea kumsimamisha uongozi bwana katule na kwamba aliitwa kwenye kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi na halmashauri ya wilaya ambapo imedaiwa kuwa alikiri kufuja pesa hizo na kuahidi atazirejesha lakini hakutekeleza hali iliypolekea kusimamishwa uongozi tangu januari 2013.
Kufuatia mvutano huo wananchi walifunga ofisi ya kijiji mwanzoni mwa wiki hii kushinikiza serikali kutatua mgogoro huo.
Mkuu wa wilaya ameagiza ofisi ifunguliwe mara moja ili shughuli za serikali ziendelee kama kawaida ambapo ofisi ilifunguliwa saa 10. 00 chini ya mtendaji kata jackson mwana na mtendaji kijiji judhith mtega.
Hata hivyo mkutano huo ulidhibitiwa na jeshi la polisi kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ambapo wananchi wamebaki hewani kwa kushindwa kutatuliwa mgogoro huo.
BAADHI YA WANAKIJIJI WA MLOWO WAKIMSIKILIZA MKUU WA WILAYA HIYO
WANAUSALAMA WAKIWA MAKINI KWA LOLOTE LITAKALOTOKEA
MWANASHERIA WA HALMASHAURI YA MBOZI AKIFAFANUA MOJA YA SHERIA ZA HALMASHAURI HIYO
YEYOTE ATAKAEZOMEA NAMTUPA NDANI HAPA NDIPO HALI YA HEWA ILICHAFUKA KWA WANAKIJIJI WA MLOWO KUMSIKIA MKUU WILAYA AKITAMKA HIVYO
MOJA YA WANAKIJIJI AKIMFUATA MKUU HUYO KUMPOKONYA KIONGELEO YAANI KAZI KUBWA
BAADHI YA WANAKIJIJI HICHO CHA MLOWO WAKITULIZWA NA BAADHI YA VIONGOZI WA KIJIJI HICHO WAPUNGUZE JAZBA
TUMECHOKA KUTUFANYA SISI WATOTO
MKUU WA WILAYA AKISHAURIANA NA MOJA YA WANAKAMATI YA ULINZI NA USALAMA MAANA MAELEWANO HAKUNA TENA KWENYE MKUTANO HUO
WANAKIJIJI HAOO WANAONDOKA MKUTANO UMEVUNJIKA HAKUNA JIBU KAMILI LILILOPATIKANA HAPO
WAKUU HAOOO NAO WANAONDOKA
KWA UJUMLA JESHI LA POLISI LINABEBESHWA MZIGO AMBAO SIO WAKE MATATIZO WAANZISHE WENGINE KUJA KUTULIZA WENGINE ENYI MNAOANZISHA MATATIZO JARIBUNI KUYAMALIZA WENYEWE MAANA HAPO MABOMU YANGEPIGWA LAWAMA INGEKUWA KWA JESHI LA POLISI HAYO NI MAONI YETU MBEYA YETU MANA TUMEONA SEHEMU NYINGI HAYA YANAFANYIKA BAADAE LAWAMA ZINAHAMIA KWA JESHI LA POLISI
WANAUSALAMA WAKIONDOKA KATIKA MKUTANO ULIOVUNJIKA
Na Kamanga Mbeya; MBEYA YETU BLOG
0 maoni:
Post a Comment