Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Jeshi la Polisi Lapiga Marufuku Maandamano ya Chadema Leo,Latoa Sababu Za Kupiga Marufuku Maandamano Hayo

Kamanda wa Polisi wa kanda ya Kinondoni ACP, Charles Kenyela

---

Jeshi la Polisi mkoani Dar es Salaam kanda ya Kinondoni limekataza maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika tarehe 16 Machi 2013 yaliyokuwa yameiratibiwa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika yaliyolenga kufika katika Wizara ya Maji ili kufikisha ujumbe kwa Waziri wa Maji, Prof Maghembe kuhusu kero ya maji katika jimbo hilo ambayo haijatatuliwa wala kupatiwa ufumbuzi kwa muda mrefu. Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo ACP, Charles Kenyela amesema endapo maandamano hayo yatafanyika:

1. Upo wasiwasi wa kutokea kwa vurugu pale watakaposhindwa kufikia muafaka kuhusu hoja zao.

2. Amewasiliana na Ofisi ya Waziri husika na kufahamishwa kuwa haina  taarifa rasmi za ujio wa maandamano hayo.

3. Barabara yatakakopita maandamano hayo ipo katika ujenzi na hivyo  maandamano hayo yatazuia shughuli za mkandarasi kukamilisha kazi yake kwa  wakati na kuisababishia Serikali hasara.

  4. Eeo ambamo maandamano hayo yanakusudiwa kutamatia ni dogo na hivyo  itasababisha usumbufu mkubwa

Taarifa kwa msaada wa HakiNgowi.Com

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO